Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

UFAFANUZI KESI YA DOWANS

 
Ufafanuzi kuhusu gharama za uendeshaji kesi ya Dowans. Juzi kwenye harambee ya M4C nilisema kwamba kabla ya kwenda Mwanza nilikuwa nafanya mahesabu ya kiwango cha gharama ambazo TANESCO imetumia na ina mwelekeo wa kutumia kwenye kesi ya Dowans pekee nikasema ni dola zaidi ya milioni 29 (ambayo ni bilioni takribani zaidi ya 40).

Nitoe ufafanuzi kwamba katika mahesabu yangu nimejumuisha USD 2.9 ml/- (takribani bilioni 4) za gharama za mawakili katika mazingira yenye utata. Na gharama za kibenki iliyowekwa Uingereza katika mazingira ya hatari ya kupoteza (risk) ya dola zaidi ya milioni 28 (bilioni zaidi ya 40) na gharama nyinginezo ambazo nitazikokotoa baadaye. Ni vizuri mkarejea hotuba niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai, 2012 ambapo nilitaja namna kesi za Dowans, IPTL, zinavyotumiwa kifisafi kama vitega uchumi kwa gharama zenye kubebesha mzigo kwa Tanesco na hatimaye wananchi kupitia bei ya juu ya umeme.

John Mnyika,
Waziri Kivuli, Wizara ya Nishati na Madini.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top