Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WALIMU WAMGEUKA MKUU WA SHULE MBUYUNI

SAKATA la uhamishaji wanafunzi kinyemela katika Shule ya Msingi Mbuyuni kwenda shule nyingine, bila kuhusisha wazazi limechukua sura mpya, baada ya walimu wa kamati ya nidhamu kumgeuka Mkuu wa shule hiyo, Doroth Malecela.
Walimu hao, wamepinga vikali kukaa vikao kujadili utovu wa nidhamu ya wanafunzi na kutoa uamuzi wa kuwahamishia shule nyingine.

Wakizungumza na MTANZANIA jana, kwa sharti la kutoandikwa gazetini walisema wamestushwa na taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Muhowera kuwa uwamuzi huo, ulifanywa na kamati ya shule hiyo.

Mmoja wa walimu hao, alisema haiwezekani kamati ya shule ikakutana na kujadili jambo ambalo lipo chini ya kamati ya nidhamu, bila wao kuhusishwa.

“Tunajua taarifa iliyopelekwa na mkuu wetu kwa Afisa Elimu ya Msingi kule Manispaa ya Kinondoni, ni ya kubuni sasa kama kweli tulikaa hebu nenda kwa Doroth akuonyeshe nakala ya vikao vyetu.

“Tumeona amesema kutokana na wanafunzi hao kufanya vitendo vibaya, suala hilo amelifikisha Ustawi wa Jamii ili kuwajengea saikolojia nzuri huo ni uongo.

“Kama kweli tulikaa na kubaini hao watoto wana matatizo, je ni hospitali gani ilidhibitisha watoto wameathirika na vitendo wanavyofanya, pia wazazi walihusishwa kwenda nao hospitali.

“Yaani tangu huyu mkuu ahamishiwe hapa, shule hii imekuwa haina amani hata sisi walimu tumegawanyika makundi mawili, ambapo moja linapinga mwenendo wake na lile linalomuunga mkono.

“Usije ukashangaa unapewa majina ya walimu bandia wa nidhamu, ukibahatika kwenda ofisini kwake jaribu kuangalia ukutani tumeorodheshwa walimu wote wa nidhamu, lakini kutokana na ujanja ujanja wa mkuu wetu, ataanza kundaa taarifa ya uongo.

“Sisi tunasema tupo tayari kuandika barua kwenda kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuelezea maovu yaliyopo hapa, hakuna asiyejua shule hii ina walimu wa vigogo, lakini tangu mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma aondoke hapa amani imepungua sana, tunafanya kazi kwa hofu,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, walimu hao wamesema hawana imani ya Halmashauri ya Kinondoni, kwa kuwa mtandao ni mmoja na mkuu wa shule hiyo, Malecela.

Alipotafutwa kwa simu, Mwenyekiti wa Kamati ya shule aliyejitambulisha kwa jina moja la Mbalinga kuzungumzia kama vikao vya kamati za shule vilikaa kujadili nidhamu ya wanafunzi, aliahidi kuzungumza na MTANZANIA leo.

Naye, Ofisa habari alipotafutwa kuzungumzia masuala hayo na mengine ambayo alishakabidhiwa alisema viongozi wote kuanzia Mkurugenzi wa Manispaa watakuwapo ofisini kuanzia Januari 3, 2013.

“Haya mambo ni vema tukawasubiri wahusika wenyewe warudi ili tupate majibu ya uhakika, mkurugenzi atakuwapo ofisini Januari 3,2013 sambamba na Afisa Elimu na Afisa Taaluma wa Shule za Msingi.

MTANZNia ilipokwenda kuzungumza na Doroth Malecela ofisni kwake, alikataa kuzungumza chochote akidai hadi atakapopata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni, Fortunatus Kwema.

Lakini baada ya mtandao huo kuwekwa wazi, Mwalimu Doroth alijadiliwa na viongozi wa manispaa hiyo, baada ya mwakilishi wa Ofisa Elimu wa Shule za Msingi, kuwasilisha tuhuma dhidi ya mwalimu huyo.

NA MTANZANIA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top