Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MEYA WA CHADEMA HATAKI MAANDAMANO,MIGOMO

MEYA wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata (CHADEMA), amesema hayuko tayari kushuhudia maandamano pamoja na migomo isiyo na tija na kuwataka wananchi kuchapa kazi kwa bidii.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na wakazi wa kata hiyo katika Viwanja vya Minazi Mitatu, kwa ajili ya kuelezea mikakati ya Manispaa yake katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili.

Alisema Manispaa hiyo bado ni changa kutokana na kuanzishwa hivi karibuni, hivyo inatakiwa kuanza kazi zake kwa kasi kwa ajili ya kushughulikia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika sekta za ardhi, nyumba, elimu pamoja na miundombinu.

Matata ambaye amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kupinga kufukuzwa uanachama na chama chake, alisema wakati huu si wakati wa wananchi wa Manispaa ya Ilemela kufanya maandamano kwa ajili ya kuwafurahisha baadhi ya watu bali ni kipindi cha kupigania maslahi ya Manispaa yao.

“Mimi sitaki kumsema mtu yeyote wala chama chochote, muhimu ninachotaka kuwaeleza wana Ilemela ni kuwa mnapaswa kupigania maslahi yenu kwanza na kuachana na maandamano ambayo yatawapotezea muda wenu bure, mie ni Meya halali wa Manispaa yenu hadi muda wangu utakapomalizika,” alisema Matata.

Alisema chini ya uongozi wake atahakikisha migogoro ya ardhi pamoja na matatizo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi yanapatiwa ufumbuzi katika muda mfupi.

“Wananchi wa Ilemela ukombozi wa kweli mtaupata kutokana na kufanya kazi kwa bidii, masuala ya kisiasa yasiwapotezee muda wenu bure, maandamano pamoja na migomo haina faida kwenu badala yake itawapotezea muda wenu bure.

“Baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwazuia wananchi kushiriki katika vikao na mikutano ya hadhara, mtapata wapi majibu ya matatizo mliyo nayo katika maeneo yenu, mnapaswa kuwaepuka viongozi wa namna hiyo kwa kuwa hawana nia njema na ninyi,” alisema Matata.

CHANZO:MTANZANIA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top