Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

HELSB YAWABURUZA KORTINI 18 KWA KUTOREJESHA MIKOPO

Wanafunzi 18 wa vyuo vikuu nchini wameburuzwa mahakamani baada ya kubainika kushindwa kerejesha mkopo uliowawezesha kupata elimu ya juu kutoka Bodi   ya Mikopo (HELSB).
Washitakiwa hao walioshitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wanadaiwa zaidi ya Sh. milioni 148.

Wanadaiwa fedha hizo ambazo walikopa kati ya mwaka 1994 na 2009 na kukubali kurejesha kwa muda ambao walikubaliana na masharti ya bodi hiyo.

Inadaiwa kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 6 C na H  cha sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004, inatamka kwamba bodi iliaminiwa kusimamia  utaratibu mzima wa kutoa na urejeshaji wa mikopo iliyotolewa na serikali tangu Julai 1994.

“Kwa mujibu wa kifungu namba 19 cha sheria ya bodi na miongozo yake, inatamka kwamba kila aliyefaidika na mkopo baada ya kukamilisha elimu yake atarejesha mkopo wa Serikali kupitia Bodi. Wadaiwa walikumbushwa kurejesha madeni kupitia vyombo vya habari, lakini walikaa kimya, hivyo bodi inaomba waamuliwe kulipa,” ilisema hati ya madai.


Bodi ya Mikopo inaomba kila mdaiwa alipe fedha alizokopa na adhabu asilimi 10 ya mkopo, alipe fidia kama mahakama itakavyoona inafaa na pia walipe gharama za kesi.

Wadaiwa katika kesi hiyo wanatakiwa kulipa jumla ya Sh. 135,132,275 ambazo ni madeni waliyokopa kwa ajili ya kuwawezesha kupata elimu ya juu na Sh. 13,513,227 ni adhabu ya kuchelewesha malipo.

Walioburutwa mahakamani ni Adam Coresh, Ally Mwenda, Anna Lymo, Hasma Tullango, Catherine  Mhina, Clement Kihamia, Dorin Lyatuu, Farida Zuku na Felix Mosha. Wengine ni Flora Peter, Frank Daniel, Harieth Mazengo, Happynes Saria, Hollo Ngeme, Mwanahamisi Abood, Ndebemeye Philipo, Ndeni Anande na Turphina Matereke.
 
CHANZO: NIPASHE
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top