TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
JAMII YATAKIWA
KUJIHADHARI NA MATAPELI WANAOPITA
MAOFISINI KUWAHADAA VIONGOZI .
Serikali inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa
hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakitumia
majina ya viongozi waandamizi wa serikali na Taasisi nyeti ikiwemo Usalama wa
Taifa kujipatia fedha kwa madai ya
kutumwa na viongozi hao.
Watu hao wamekuwa
wakituma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa maofisa mbalimbali wa wizara, mashirika
ya umma na Idara za Serikali zinazojitegemea kuomba pesa ili wawafanye mipango
ya kupandishwa vyeo.
Utapeli huo
umekuwepo nchini kwa kipindi kirefu sasa , ambapo watu huwapigia simu viongozi
wa Taasisi za fedha , Mifuko ya Taasisi za Jamii na watu binafisi wakiomba
fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi waandamizi Serikalini wakati si kweli.
Watu hao wamekuwa
wakiwatapeli maofisa mbalimbali kuwa wanaweza kuwafanyia mipango ya kupandishwa
vyeo endapo watawapatia kiasi cha fedha jambo ambalo halipo katika taratibu za
utumishi wa umma.
Utumishi wa
umma unazo taratibu zake za kuwapandisha vyeo watumishi wake kulingana na sifa
za kada zao na wala haiwezekani kwa viongozi waandamizi kuwachangisha fedha kwa
ajili ya kuwapandisha vyeo.
Serikali
inawataka wananchi kuwapuuza matapeli hao na watoe taarifa katika vyombo vya
dola na usalama mara wapatapo ujumbe wa aina hiyo ili hatua zichukuliwe dhidi yao.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI (MAELEZO) DAR ES SALAAM.
12.02.2013
Post a Comment