Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) akibadishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume, Dkt. Sengondo Mvungi nje ya ukumbi wa Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume leo Ijumaa (Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga alikutana na Wajumbe ili kubadilishana mawazo na uzoefu katika uandishi wa Katiba Mpya.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (kushoto)
akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga nje ya
ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano
kati yake na Wajumbe wa Tume leo (Ijumaa Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga
amekutana na Wajumbe wa Tume kubadilishana mawazo na uzoefu wake kuhusu
uandishi wa Katiba Mpya.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akimwonyesha nakala ya Kitabu
Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) nje ya ofisi za Tume
mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wajumbe wa Tume baina
yao uliofanyika katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa
Feb. 15, 2013). Mhe. Mtungi amekutana na Wajumbe wa Tume kuzungumzia
uzoefu wake kuhusu uandishi na utekelezaji wa Katiba Mpya. Kulia ni
Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba.
(PICHA NA TUME YA KATIBA)
Post a Comment