Matokeo
yaKidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri)
na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la
sifuri ni mwaka tatu sasa mfululizo. Matokeo yakitoka tunasema weeee
mpaka povu linatoka. Baada ya wiki tumeshasahau na hakuna hatua yeyote.
Lazima Uwajibikaji utokee.
kwanza Waziri lazima awajibike na
Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna. Najua kuwa haina uhusiano wa moja
kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa sana nchini. Lakini ni
lazima kitu fulani kitokee ili kufanya mabadiliko. Uwajibikaji ni njia
mojawapo inayoleta nidhamu na 'urgency' katika utendaji kazi.
Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye
(kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki
hivi mwakani na yeye atatoka. Najua wa mwakani ndio wapo kidato cha nne
sasa na wana msingi mbaya tayari lakini sio jukumu letu kujipa majibu
bali ni jukumu letu kuiambia Serikali hapana. Tuwape Masharti.
Vinginevyo haya yatakwisha na mwakani itakuja nk.
Hawa watoto
wanakwenda wapi? Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo vya ufundi
kila Halmashauri ya Wilaya uanze mara moja. Katika Bajeti Kivuli mwaka
2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji tshs 720 bilioni katika kipindi
cha miaka 5 ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA kila Wilaya.
Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kulipana
posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana Elimu ni Hifadhi ya
Jamii. Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwneye jamii na ni hatari
sana kwa uhai wa Taifa.
Tunaweza kujidai kujenga madaraja na
miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na kusambaza umeme
kila kijiji mpaka kwenye vyoo. Kama hakuna Elimu haya yote ni bure
kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa mbaya zaidi
unapokuwa na Taifa la mambumbumbu. Waziri Kawambwa na wenzake watoke.
Watoke SASA
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Tuesday, February 19, 2013
Post a Comment