Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MHE.MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akiwa na Naibu wake Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) walipokutana kwa mazungumzo  na ujumbe kutoka Jamhuri ya Watu wa China ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Zhai Jun (hayupo pichani)

Mhe. Membe na Mhe. Maalim wakiendelea na mazungumzo na ujumbe huo kutoka China kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na China. Kulia kwa Mhe. Membe ni Balozi Rajabu Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Zhai Jun (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Mhe. Lu Youqing (kulia), Balozi wa China hapa nchini na Bi. Zhang Jing, Mkalimani wa ujumbe huo.

Mhe. Zhai Jun, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China akizungumza na Mhe. Membe (hayupo pichani) na wajumbe wengine.

Mhe. Membe na Mhe. Maalim wakimsikiliza Mhe. Zhai Jun (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Wajumbe  wa Tanzania wakati wa mazungumzo hayo.

Mhe. Membe akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo huku Mhe Zhai Jun na wajumbe wengine wakisikiliza

Wajumbe wa China na Tanzania kwa pamoja wakimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo hayo.


Wajumbe wengine wa Tanzania waliokuwepo kwenye mazungumzo hayo. Kulia ni Bw. Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Mhe. Membe akimsindikiza Mhe. Zhai Jun mara baada ya mazungumzo yao

Mhe. Membe akiagana na Mhe. Zhai Jun.

Mhe. Membe akiteta jambo na Balozi Lu Youqing mara baada ya mazungumzo huku Mhe. Maalim akisikiliza kwa makini.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top