Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la
Askofu Mstaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus
Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu
Mfalme, mjini Moshi juzi
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu
Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie
wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme
mjni Moshi juzi
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu
Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie
wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme
mjini Moshi juzi
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni (KUB) akitoa heshima zake za mwisho kwa Askofu Mstaafu
wa Kanisa Katoliki nchini, hayati Amedeus Peter Msarikie, katika misa ya
kumuaga iliyofanyika jana katika Kanisa la Kristo Mfalme, Mjini
Moshi.Picha na Freddy Maro-IKULU
---
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete juzi, Alhamisi,
Februari 14, 2013 ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa
Katoliki, Jimbo la Moshi na kutoka sehemu nyingine nchini, kumzika
Askofu Mstahivu (Bishop Emeritus) Amedeus Peter Msarikie.
Rais
Kikwete aliwasili kwenye Kanisa Kuu la Kristo Mfalme mjini Moshi kiasi
cha saa sita na dakika tano mchana kuungana na marais wastaafu Ali
Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na mamia kwa mamia wananchi kwa ajili ya
mazishi ya Askofu Msarikie ambaye alifariki dunia Alhamisi iliyopita,
Februari 7, 2013 kwa ugonjwa wa saratani katika hospitali moja mjini
Nairobi, Kenya.
Mara baada ya kuwasili, Rais Kikwete alitia saini
kwenye kitabu cha maombolezo na ikaanza ibada ya mazishi
ilivyohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi wakiwamo maaskofu zaidi
ya 20 kutoka majimbo mbali mbali ya Kanisa Katoliki nchini.
Mwili
wa Marehemu Msarikie uliteremshwa kaburini kiasi cha saa saba na dakika
35 ndani ya Kanisa hilo na Rais Kikwete akaweka udogo kwenye kaburi na
baadaye shada la maua.
Akizungumza kwenye mazishi hayo, Rais
Kikwete amemwelezea Askofu Msarikie ambaye alikuwa Askofu wa Jimbo la
Moshi kwa miaka 26 kama “kiongozi shupavu wa kiroho ambaye aliwalea
vyema kondoo wa bwana. Lakini pia alikuwa kiongozi hodari kwa maendeleo
ya jamii yaliyowanufaisha waumini wake na hata wale wa madhehebu na
dini nyingine.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Kwa kweli sote
tumepoteza mtu muhimu. Tunamfahamu marehemu Baba Askofu Msarikie kwa
mema mengi aliyowatendea watu wa jimbo lake, ya kiroho na ya maendeleo.
Mimi binafsi, wana-moshi na Watanzania kwa ujumla tutamkumbuka na
kumuenzi Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowafanya wanadamu
wenzake na nchi yetu.”
Taarifa kwa hisani ya Gadiola Emmanuel
Post a Comment