Msafara wa rais Jakaya Kikwete ukiwa
umesimama kwa muda eneo la msitu wa taifa wa Sao Hill Mufindi
katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya kufuatia moto mkubwa kuwaka
katika msitu huo mchana wa leo
Askari polisi akimamisha msafara wa
rais Kikwete kutokana na moto mkubwa kutanda eneo hilo la Changalawe
katika msitu wa Taifa wa Sao Hill umbali wa mita mbili kuelekea
barabara ya Ikulu ndogo mjini Mafinga
Askari wa FFU wakishuka katika gari
lao kwenda kuangalia usalama wa rais Kikwete na kulia gari la kwanza
ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili la la tatu ni magari ya Ikulu
yakiwa yamesimama
hapa askari wakishuka kuingia katika
moshi mzito kuangalia usalama wa rais katika eneo hilo ambalo moshi
mzito ulitanda barabarani
Msafara ukipita eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto huo
Huu ndio moto unaoendelea kuteketeza msitu wa taifa wa Sao Hill Mufindi .
SOURCE:Iringa yetu Blog