Wanajeshi wa Serikali wakishika doria nchini Misri
..........
Utawala nchini Misri, umeishutumu, vugu vugu la
Muslim Brotherhood, lililopigwa marufuku kwa kuunda kitengo maalum cha
kijeshi Kusini mwa nchi hiyo, ili kufanya mashambulio dhidi ya wanajeshi
wa serikali.
Wizara ya usalama wa ndani nchini Misri, imetoa
orodha ya majini ya watu kumi na wawili wa kitengo hicho, na kuwashutumu
kwa kuwauawa maafisa watano wa polisi katika mkoa wa Beni Suef.
Maafisa wa Ulinzi nchini Misri wamewauawa
takriban wafuasi elfu moja wa vugu vugu hilo la Muslim Brotherhood,
tangua jeshi la nchi hiyo lilipomuondoa madarakani, rais Mohamed Morsi
Julai mwaka uliopita.
Kundi hilo limesema kuwa linapinga vikali ghasia
na machafuko, lakini kumekuwa na mashambulio kadhaa dhidi ya maafisa wa
ulinzi yanayotekelezwa na watu wanaoaminika kuwa wapiganaji wa
Kiislamu.
Awali siku ya Jumapili, kiongozi mmoja
mwandamizi wa Kiislamu, Abdel Moneim Aboul Fotouh alisema kuwa, taifa la
Misri limegeuka na kuwa Jumuhuri la uoga.
NA BBC SWAHILI

Post a Comment