Meneja
Mkuu wa SuperSport kwa ukanda wa Kusini mwa Afrika, Graeme Murray
akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika
(hawapo pichani) katika hoteli ya OutriggerHotel & Beach Resort
nchini Mauritius.
Na Modewjiblog, Mauritius
WAKATI
leo michezo ya 11 ya All African games chaneli ya SuperSport imetangaza
rasmi kwamba watashika usukuni wa kurusha matangazo ya michezo hiyo
kupitia SuperSport 9 Michezo hiyo imeanza juzi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa uzalishaji wa SuperSport, Alvin Naicker
wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkusanyiko mkubwa wa
MultiChoice uliohusisha waandishi wa habari, masupastaa na chaneli
wanazofanya kazi nazo katika hoteli ya OutriggerHotel & Beach Resort
nchini Mauritius.
Akiwa
mtu kati Naicker alisema kwa kujiamini kwamba urushaji wa matangazo
hayo ni sehemu ya uuzaji wa sura ya michezo ya Afrika katika mabara
mengine.
Akiwa
katika mazungumzo hayo ambayo yalioongozwa na mmoja wa watu wanaotoa
burudani kubwa ya utangazaji ndani ya SuperSport, Carol Tshabalala
alisema hali hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta
nzima ya burudani na michezo na kampuni ya MultiChoice.
Mkuu
wa masoko wa SuperSuport, Motheo Matsau akifurahia jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari katika visiwa vya Mauritius.
Katika
mazungumzo hayo ambapo pia alikuwapo Mkuu wa masoko wa SuperSuport,
Motheo Matsau, Meneja mkuu wa SuperSport kwa ukanda wa Kusini mwa
Afrika, Graeme Murray na mgeni maalum Anthony Baffoe, mchezaji wa
zamani wa kimataifa na Mratibu mkuu wa FIFA na CAF, Naicker alisema
ubora wa chaneli yake unatokana na kuweza kunoa vipaji vya watangazaji
wake kufikia kiwango cha juu kabisa cha ubora.
Kama mwekezaji mkubwa wa masuala ya michezo katika bara la Afrika, SuperSport imepata matokeo ya kuridhisha na yenye tija.
“Mwaka 2006 tulipeleka kundi dogo la watu 26 Abudja kutangaza mpira
lakini leo hii tunaringia kuwa na asilimia 100 ya watangazaji wenyeji
wakifanyakazi zao katika nchi za Nigeria na Ghana,”alisema Murray.
Baffoe
naye aliongeza kwamba mchango wa SuperSport umeongeza zaidi ya
utangazaji na kuwezesha kuongezeka kwa kiwango cha uprofesheni katika
ligi mbalimbali barani Afrika.
Mchezaji
wa zamani wa kimataifa na Mratibu mkuu wa FIFA na CAF, Anthony Baffoe
akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
“SuperSport
iliweka msingi wa utoaji leseni kwa klabu, kuwaelimisha watawala,
kuweka viwango vya msingi katika viwanja, kusaidia kuanzishwa kwa umoja
wa wachezaji, kuwafanya wachezaji kuwa wadau muhimu katika ligi na
kuwaruhusu wajipange kwa maisha nje ya soka,” alisema.
Murray
alielezea jinsi watangazaji walivyoweza kujishirikisha katika ligi za
wenyeji kama mfano bora namna ambavyo Supersport imesaidia michezo
katika bara hili
“Tulianza kushirikiana na Ligi Kuu ya Nigeria mwaka 2006 na imeendelea
kukua mwaka hadi mwaka,” alisema. “Tuliweza kuingia katika Super Eagles’
League ya Nigeria na ligi ya kikapu ya Nigeria, ligi zote mbili
zinafanya vyema kuliko hapo awali.Tumekuwa washirika wa Ligi Kuu ya
Kenya kuanzia mwaka 2008 na Ligi Kuu ya Ghana toka mwaka 2012. Inatakiwa
kukumbukwa kwamba kabla ya kuingia kwetu Kenya hakuna hata mechi moja
ya ligi iliweza kutangazwa katika runinga na sasa ligi inazidi kukua.”
Mkuu wa uzalishaji wa SuperSport, Alvin Naicker akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Aidha
SuperSport katika siku za karibuni imekamilisha mkataba na waendeshaji
wa Ligii kuu ya Zambia kuendelea kuonekanakana katika Supersport kwa
miaka mitano ijayo.
Aidha chaneli ya SuperSport inajipanga kuanzisha jarida nchini Zambia litakalouza soko la Zambia kwa mataifa ya Afrika.
Mkuu
wa masoko wa SuperSport, Motheo Matsau pia ameongeza kwamba
kunahitajika kuuza kwa michezo bara la Afrika na kwa yakini kama
maendeleo yaliyopo hayataonekana kwa dunia , itakuwa hakuna maana,
kinachojalisha ni kwa kadamnasi ya kimataifa kujua kwamba Afrika ina
vipaji bora kabisa katika michezo.
Alisema
kupitia matangazo ya chaneli hiyo kunaonesha kwamba mauzo yanaleta
faida kama ulivyo mchezo wenyewe na hilo ndilo linafanya Super Sport
kuwa chaneli bora zaidi duniani.
Wakati
mtu akitoka katika mafunzo ya utangazaji ya chaneli hii anajua michezo
na ajui namna ambavyo masuala ya utangazaji yanavyofanyakazi. Watu hawa
wanakuwa mabalozi wetu na vyanzo muhimu sana vya habari.Tunatia
SuperSport uhai kwa kuwakutanisha watu hawa.”
Naicker katika mazungumzo hayo alisisitiza kuendelea kuwepo kwa
mahusiano mazuri kati ya SuperSport na wadau wa michezo wa bara la
Afrika.
“Sisi si kwamba tunalipa fedha kwa ajili ya kupata kibali cha kutangaza
au kupiga picha za video tukio la burudani hii, lazima kuwepo na utoaji
wa elimu, mchakato unaostahili kukabiliwa na pande zote mbili.
Tunapaswa
kujua muda gani unastahili kuchezwa na mambo gani ambayo hayastahili
kuyatangaza. Tumetengeneza kijarida cha utangazaji ili kila mmoja aweze
kusoma kuwasaidia wengine katika mchakato wa namna matangazo
yanavyorushwa na ushawishi wake lojistiki, usahihi wa muda na upangaji
fixtures. Tunataka ujenga ushirikiano wenye ufanisi kwa muda mrefu,”
alisema.
Naicker pia alitumia nafasi hiyo kuelezea furaha yao ya kupata zabuni ya kutangaza michezo ya olimpiki ya mwaka 2016.
Carol Tshabalala wa Supersport akiendesha mkutano na waandishi wa habari.
“Tutakuwa chaneli nyingi za michezo hiyo, kiwango cha chini kabisa zikiwa ni chaneli 6 kwenye SuperSport bouquet,” alisema.
“Tutarusha
kila tukio ambalo mwafrika ana nafasi ya kutwaa medali. Tumetengeneza
makundi ya watangazaji na timu zao kufuatilia timu za Kiafrika katika
tukio hilo kubwa. Aidha tayari tumeshaanza mazungumzo na mamlaka kubwa
za michezo katika nchi za bara la Arika kujua watu ambao wanaweza kutwaa
medali ili kuanza kuandaa stori zao kuelekea michezo ya Olimpiki.”
“Tunajivunai si tu kuwa watangazaji wazuri wa michezo katika bara la Afrika, bali duniani,” anasema Naicker.
Kwa
kuwatumia masupastaa wa Afrika kama akina Sammy Kuffour kuelezea
masuala ya kiufundi na utaalamu wa ndani unachokiona, kusaidia kunyanyua
michezo kutoka katika ngazi za awali chini kabisa kwa kuwa na miradi
maalumu, SuperSport inaongoza katika kuelezea mafanikio ya Afrika katika
michezo kwa mataifa mengine duniani.
Mwandishi
wa habari hizi na wengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika wapo nchini
Mauritius katika moja ya maonesho makubwa ya watoa burudani kwa njia ya
televisheni na video ya MultiChoise wanaotumia mtandao wa DSTV na GoTv.
Carol Tshabalala wa SuperSport.
Post a Comment