JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
Taarifa
za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania waliopotea huko Saudi
Arabia
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea majina
18 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawaonekani kufuatia tukio la
mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba,
2015 na kusababisha vifo vya watu 769 na wengine 934 kujeruhiwa.
Itakumbukwa kuwa tarehe 28 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa
kuwa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana huku wengine watano
wakiwa wamefariki dunia.
Majina ya baadhi
ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-
1. Abdul Iddi
Hussein
2. Awadh Saleh
Magram
3. Burhani
Nzori Matata
4. Yussuf
Ismail Yusuf
5. Saleh Mussa
Said
6. Adam Abdul
Adam
7. Archelaus
Antory Rutayulungwa
8. Farida
Khatun Abdulghani
9. Rashida
Adam Abdul
10. Hamida
Ilyas Ibrahim
11. Rehema
Ausi Rubaga
12. Faiza
Ahmed Omar
13. Khadija
Abdulkhalik Said
14. Shabinabanu
Ismail Dinmohamed
15. Salama
Rajabu Mwamba
16. Johari
Mkesafiri Mwijage
17. Alwiya
Sharrif Salehe Abdallah
18. Hafsa
Sharrif Saleh Abdallah
Mbali na
taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa
kwa mwili wa hujaji mmoja wa Tanzania anayeitwa Hadija Shekali Mohammed wa
kikundi cha Ahlu Daawa.
Aidha, Serikali ya
Saudi Arabia imetoa picha za maiti za Mahujaji waliokufa Makkah ambao
wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi. Hivyo,
Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya Mahujaji unaendelea na
zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za Mahujaji
wetu waliopotea.
Vilevile,
Mamlaka ya Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa imechukua alama za vidole za
Mahujaji waliokufa ili wazilinganishe na zile walizozichukua Uwanja wa Ndege
wakati Mahujaji hao wakiingia nchini humo. Wizara inaamini kuwa taarifa za
alama za vidole zitakapotolewa zitasaidia sana kuwatambua Mahujaji wetu.
Pamoja na
jitihada zote hizo, Ubalozi pia unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji
wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali
zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
29 Septemba, 2015
Post a Comment