Tanzania na Kenya zimeanza kampeni ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwa ushindi.
Tanzania imeicharaza Malawi 2-0 katika mechi iliyochezewa uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mukapa jijini Dar es Salaam.
Bao la kwanza la Taifa Stars limefungwa na Mbwana Samata dakika ya 18 na la pili na Thomas Ulimwengu dakika ya 22.
Nchini Mauritius, Kenya walikuwa na mteremko, wakiondoka na ushindi wa 5-2 dhidi ya wenyeji wao.
Harambee Stars ilitangulia kufunga kupitia Johanna Omolo dakika ya 18, Ajub Masika dakika ya 23 na Shakava dakika ya 49.
Mauritius hata hivyo walijikakamua na nusura wafanye mapinduzi baada ya
kupata mabao mawili kupitia Sophie dakika ya 66 na Bru dakika ya 78.
Lakini Kenya walidhibiti tena mchezo kupitia bao la Michael Olunga dakika ya 87 na bao la pili la Omolo dakika ya 82.
Mechi kati ya Sudan Kusini na Mauritania, ambayo ilikuwa yao ya kwanza
kabisa katika dimba la Kombe la Dunia, ilisimamishwa kutokana na mvua
kubwa.
Wakati wa kusimamishwa kwa mechi hiyo mjini Juba, timu zote mbili
zilikuwa sare 1-1, bao la Sudan Kusini likitoka kwa Dominic Abui Pretino
na la Mauritania Boubacar Bagili.
Katika mechi nyingine, Burundi walilaza Ushelisheli kwa bao moja bila
Post a Comment