o
Mkurugenzi
wa Mafunzo na Uelimishaji Kitaifa kutoka kampuni ya SBC Tanzania,
Rashid Chenja akionesha tangazo jipya linaloonyesha punguzo la bei ya
soda zao kutoka Tsh. 600 hadi Tsh. 500 kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) bei ambayo inaanza kutumika sasa kuanzia leo. Wengine: Kushoto
ni Roselyne Bruno Meneja Masoko wa kampuni hiyo na kulia ni Omary
Mandaya Meneja mauzo wa kampuni hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Rabi Hume,Modewjiblog
Kampuni
ya kutengeneza vinywaji ya SBC Tanzania imeshusha bei ya vivywaji vya
Pepsi, Milinda, Mountain Dew na Mountain Dew kutoka shilingi 600 hadi
500 kwa ujazo wa milimita 350 na 300 na milimita 250 kuwa shilingi 400.
Akitangaza
kushuka kwa bei hiyo, mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
mafunzo na uelimishaji kitaifa kutoka SBC, Rashid Chenja amesema sababu
ya wao kushusha bei ya vinywaji vyao bei ni kuwapa nafasi wateja wao
kutumia bidhaa hiyo kutokana na hali za kimaisha kuzidi kupanda.
Amesema
kabla ya kufikia uamuzi huo walifanya utafiti kwa kuzunguka maeneo
mbalimbali na kuchukua maoni ya watumiaji wa vinywaji vyao ambao wengi
wao walipendekeza bei ya shilingi 500 kutokana na hali za kimaisha kuwa
ngumu na pia 500 ni pesa ambayo haina usumbufu mkubwa hata katika
upatikanaji wa chenji.
“Kabla
hatujaja hapa kutangaza bei zetu mpya tulifanya utafiti kwenye sehemu
mbalimbali kuhusu kinywaji chetu na wengi wametoa maoni wakitaka bei
ishuke hali ya maisha ngumu na hata hivi 500 haisumbui kupata chenji
hivyo tunatangaza rasmi kushusha bei ya vinywaji vyetu,” amesema Chenja.
Ameitaja
mikoa ambayo inanufaika na punguzo hilo kuwa ni Dar es Salaam,
Morogoro, Dodoma, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara na Zanzibar ambapo kwa
sasa wauzaji wa bidhaa zao wameomba wamalize bidhaa walizokuwa nazo
ndiyo waanze bei mpya na watakuwa wakinunua kreti moja kwa 9,400 na
watakuwa wakipata faida ya 2,500.
Nae
Meneja masoko wa SBC Tanzania, Roselyne Bomio amesema licha ya kushusha
bei ya vinywaji hivyo pia wapo katika mchakato kuona jinsi wanavyoweza
kushusha bei ya vinywaji vyao vya milimita 500 ambavyo kwa sasa vinauzwa
shilingi 800 licha ya maeneo mengi kuwa wakiuza 1,000.
Mkurugenzi wa Mafunzo na
Uelimishaji Kitaifa kutoka kampuni ya SBC Tanzania, Rashid Chenja
akisisitiza jmbo juu ya bei za soda zao kutoka Tsh. 600 hadi Tsh. 500
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) bei ambayo inaanza kutumika
sasa kuanzia leo. Wengine: Kushoto ni Roselyne Bruno Meneja Masoko wa
kampuni hiyo na kulia ni Omary Mandaya Meneja mauzo wa kampuni hiyo.
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo..
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo..
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo la mapema le
Post a Comment