Kikao cha Kamati ya wabunge wa CCM kilichofanyika usiku wa kuamkia leo
katika ukumbi wa NEC maarufu kama Whitehouse kimempitisha Dkt Tulia
Ackson Mwansasu kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi katika nafasi ya
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamati ya Uongozi ilipitisha majina matatu ya Mhe Bahati Abeid, Mhe Mariam Kisangi na Dkt Tulia Ackson Mwansasu ambapo Dkt Tulia aliibuka mshindi baada ya wawili kujitoa na kumuunga mkono Dr Tulia.
Dk Tulia awali alikua akigombea nafasi ya Spika kabla ya kuingia katika mtanange wa Naibu Spika.
Aidha Naibu Mwanasheria huyo wa zamani aliteuliwa juzi na Rais Dk John Magufuli kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais.

Post a Comment