Simba ni ikiwa imechimbia Kileleni mwa Vodacom Premium League Uongozi wake umetoa rai kwa mashabiki wa klabu hiyo kutowazomea wachezaji wa Yanga watakapokuwa wanaiwakilisha Tanzania kwenye mechi ya kombe la vilabu bingwa Afrika Jumamosi dhidi ya St. Louis Suns United kwenye uwanja wa taifa.
Hilo limesemwa na Afisa habari wa Simba Haji Manara, ''hawana undugu na Yanga lakini mashabiki wa Simba wasiwazomee kwa sababu watakuwa wanawakilisha nchi''.
“Nawaomba mashabiki wa Simba wasiende kuizomea Yanga kwenye mechi yao ya kimataifa siku ya Jumamosi, kama hawawezi wasiende uwanjani. Sisi sote ni wawakilishi wa nchi, tunapofungwa na timu kutoka nje hawasemi wameifunga Yanga au Simba wanasema wameifunga Tanzania”-Haji Manara.
“Yanga si maadui zetu, ni watani zetu, ‘kucharurana’ kubaki kwenye mechi zetu za hapa nyumbani, kama wao watatuzomea ni wao siwezi kuwaomba wasifanye hivyo.”
Msemaji huyo mwenye maneno mengi amesema Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassani Mwinyi atakuwa mgeni rasmi kwenye mechi yao ya Caf Confederation Cup dhidi ya Gendarmerie Nationale siku ya Jumapili kwenye uwanja wa taifa.
Klabu hiyo ya Simba imetangaza viingilio kwa ajili ya mchezo huo ambapo kiingilio cha chini kabisa kitakuwa ni Tsh. 5000 kwa viti vya mzunguko.Hii ni katika kuwavutia mashabiki wengi kuingia ili kuipa hamasa timu ikicheza.
Katika majukwaa mengine Viingilio vitakuwa ni VIP A Tsh. 30,000, VIP B Tsh. 20,000, viti vya Orange Tsh. 10,000.
Simba ambayo imekosekana katika Soka la Kimataifa kwa muda mrefu inauchukulia kwa umakini sana mchezo huo.
Post a Comment