Wilshere, mwenye Miaka 26, amekwama kwenye mazungumzo na Arsenal. lakini rekodi yake mbaya ya kuumia mara kwa mara inaonyesha mkataba wake mpya utategemea sana na pafomansi yake uwanjani.
Lakini Jurgen Klopp yupo tayari kumpa Wilshere mkataba wake wa sasa mwishoni mwa msimu akiwa mchezaji huru.
Klopp tayari ameshamchukua mchezaji mwingine wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain kwenye dili la pauni £35 milioni.
Na inajulikana kwamba amekuwa akimuhusudu Wilshere ambaye anapambana kurudi kwenye timu ya Taifa ya Uingereza ili ashiriki World Cup.
Mjerumani huyo anamuhitaji kiungo huyo ili kuweza kuziba pengo Emre Can ambaye anaonekana kuvutiwa na Juventus.
Can hajakubali kusaini kandarasi mpya Anfield na Klopp amesema: “Wakati mwingine mchezaji anapenda kuona mkataba wake unafika mwisho, hili sio jambo zuri kwa Klabu ,lakini kipindi inabidi uikubali hali hiyo"
Gwiji wa Liverpool Phil Thompson anaona Wilshere utakuwa ni usajili mzuri sana kwa wekundu hao.
Alisema: “Ningemchukua kuja Liverpool — ana uwezo mkubwa .”
“Nimekuwa nikimhusudu kwa muda mrefu.”
Maoni yake yaliungwa Mkono na mchezaji wa zamani wa Arsenal staa Paul Merson ambaye alisema: “Nadhani Liverpool watamchukua sio muda mrefu.”
Post a Comment