*Mashabiki wamtupia lawama kocha Antonio Conte.
Watford walifunga magoli matatu dakika za mwisho ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Javi Gracia katika uwanja wa nyumbani katika usiku ambao hautasahaulika na kuzidi kuongeza presha kwa Kocha Antonio Conte wa Chelsea.
Timu hiyo inayofahamika kwa jina la 'The Blues' walicheza karibu saa nzima wakiwa pungufu watu 10 baada ya Tiemoue Bakayoko kupewa kadi nyekundu baada ya kucheza madhambi dakika ya 30 ya mchezo iliyopelekea Watford kupata nafasi nne.
Watford ambao wameshinda mara katika michezo 12 iliyopita waliongoza baaada ya kupata penati kwa Gerard Deulofeu kujiangusha kirahisi wakati akikabiliana na Kipa Thibaut Courtois' na Troy Deeney kufunga penati hiyo..
Katika dakika ya 84 Daryl Janmaat alifunga goli la pili zuri baada ya kutoka winga ya kulia kucheza 'one-two' Roberto Pereyra na kuwapita walinzi kadhaa wa Chelsea na kufunga kwakutumia mguu wake wa kushoto.
Deulofeu aliongeza goli lingine katika dakika ya 88 baada ya kukimbia na mpira kutoka katikati ya Uwanja na kupiga shuti lililombabatiza Gary Cahill kabla ya Pereyra kufunga goli la nne.
Magoli ya Watford yalifungwa na Deeney dakika ya 42,Janmaat 84,Deulofeu 88 na Pereyra 90
Wakati lile la Chelsea lilifungwa na Hazard 82
Watford wapo na pointi sita zaidi kutoka kwenye timu zilizo kwenye hatari ya kushuka daraja.
Magoli ya Watford yalifungwa na Deeney dakika ya 42,Janmaat 84,Deulofeu 88 na Pereyra 90
Wakati lile la Chelsea lilifungwa na Hazard 82
Watford wapo na pointi sita zaidi kutoka kwenye timu zilizo kwenye hatari ya kushuka daraja.
Gracia, aliyechukua mikoba Marco Silva mwezi uliopita , aliviambia vyombo vya habari kuwa "Ni ushindi mkubwa sana na mechi muhimu sana.Ninaona fahari kwa wachezaji wangu siku ya leo.
"Tumecheza mchezo mzuri,tuliwashambulia.Na mechi ilibadilika baada ya kutolewa nje Bakayoko,nafikiri tulicheza vizuri. Chelsea ni timu kubwa na klabu kubwa."
Ni mcheoz wa pili mfululizo kwa kufungwa Chelsea baada ya kipigo 3-0 nyumbani na Bournemouth.
Na Chediel Charles
Kwa Msaada wa Mitandao.
Post a Comment