Loading...
SIMBA KUKIPIGA AL MASRY MWEZI MACHI 2018
Wekundu wa Msimbazi Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendarmarie Nationale FC, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho , Simba sasa itacheza na Al Masry SC March 6 2018.
Simba inaingia hatua hiyo mara baada ya Simba kufikisha jumla ya mabao 5-0 katika Aggregate.
Simba ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuwakaribisha Al Masry hapa nchini, mchezo ukipigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Saalam.
Baada ya mechi hiyo, mchezo wa marudiano utachezwa March 16 2018 katika Uwanja wa Al Masry Club, utakaochezwa nchini Misri.
Masry wanakutana na Simba baada ya kuiondoa Gren Buffaloes kwa jumla ya mabao 5-2.
Chediel . Powered by Blogger.
Post a Comment