Saturday, July 25, 2009

Bwawa la maini

Mashabiki wa Bwawa la maini wakiwa kwenye wanja lao hapo juu.
Katika pitia pitia mtandaoni nikakutana na habari hii ya wanachama hao kujipanga ili waweza kumiliki chama lao kama Barca na klabu nyingine Ulaya wanavyomiliki.Hatujui mwisho wake nini ...pata kwa undani zaidi.

SHARELIVERPOOLFC MAKE REVISED PROPOSAL
PRESS RELEASE

SHARELIVERPOOLFC MAKE REVISED PROPOSALFOR FAN BUY OUT, SUPPORTED BY SPIRIT OF SHANKLY
On the deadline day for the American owners of Liverpool FC to complete the refinancing of the debt they took on to buy and run the Club, the two key supporters’ groups, ShareLiverpoolFC (SLFC) and Spirit of Shankly (SoS) unveiled a revised fan buy-out plan for consideration by the banks and the owners. Though it is expected that RBS & Wachovia will extend the credit line to the current owners, in the view of the fans, this is only a short term (and expensive) fix for LFC.
Initially SLFC looked to raise £500m from 100,000 LFC fans who would pay £5,000 for a single share. Feedback received from SLFC registrants and SoS has convinced SLFC that reducing the ‘entry fee’ from £5,000 to £500 is the best way forward, as it ensures a much broader base of fans can get involved. Subsequently, they have put together a revised proposal.
The revised proposal is designed to achieve:
Fan ownership of Liverpool FC

A much broader base of that ownership by reducing the entry price for a single share from £5,000 to £500
One member: one vote

A way in which fans who can afford to put in more than £500 can receive a return of 2%
A way commercial investors can participate

The fan groups are looking to raise £150 million from LFC fans to initially acquire a 60% interest in the Club:
Approximately £10 million to come from the sale of £500 shares in ShareLiverpoolFC on a one person one share basis

Approximately £140 million to come from shareholding fans acquiring SLFC Loan Stock which gives them a return of 2% a year
In addition to this, they are seeking a commercial partner to invest £100 million in return for a 40% interest in the Club, through a combination of loan stock and equity shares. This raises in total £250 million which can be used to pay down £250 million of the current £350 million of bank debt.
The £100 million balance of current bank debt would be exchanged for convertible loan stock in LFC, which SLFC would have rights to acquire from the banks in equal annual instalments over a 20 year term. Acquisition and conversion of the LFC loan stock would eventually raise SLFC’s equity interest in the Club to 71%.
The SLFC Board issued the following statement:
“This is a realistic plan that squares the circle: How to get broadly based fan ownership of the Club, and relieve the level of debt, by offering Liverpool fans an affordable entry fee and a chance to get a modest return for their additional financial support. Now we need all those Liverpool fans to carefully consider the proposals in detail on our website – and let us know what they think”.

A Spirit of Shankly spokesperson added: “This new proposal is a sound, sensible and workable plan which offers the only real solution for the Club: long term financing that isn’t supported by short term – and expensive - bank debt. The new proposal can do precisely that.”
Supporters Direct Chief Executive, Dave Boyle, said:
“This proposal is the only sensible, sustainable offer that’s been put forward that also meets the crucial community requirements. Community ownership is something both the Government and UEFA are strongly supportive of, and this proposal is very much in line with that. The Club seems to be at a crossroads. It will either continue to be owned by a group of distant people with an eye on the bottom line, driven by the need to pay off colossal debts, or owned by the community, like Barcelona or Bayern Munich
.”
Credit to:
http://www.shareliverpoolfc.com/

Haile Selassie Kukumbukwa Leo

Chama cha marasta Tanzania kinakukaribisha katika sherehe za kumbukumbu za Haile Selassie leo hapa Jijini Dar es salaam,Mitaa ya Mwenge katika ukumbi wa Kilimanjaro 2000.
Picha kwa hisani ya Nifahamishe.com

Thursday, July 23, 2009

TAMASHA LA SAUTI YA KISWAHILI (TASAKI)

CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii
Idara ya Lugha na Fasihi- Kitengo cha Kiswahili


TAMASHA LA SAUTI YA KISWAHILI (TASAKI)

Lugha ya Kiswahili sasa imevuka mipaka ya kitaifa. Ni lugha ambayo imeshuhudia mageuzi mengi na imepiga hatua kubwa sana. Tunashudia watu wengi ulimwenguni wakijifunza Kiswahili na hata Vyuo Vikuu vikifundisha Kiswahili. Ni wakati ambao watanzania tunahitaji kukipa kipaumbele na kujivunia lugha yetu na utamaduni wake, kuipa nafasi na dhima maalumu katika nyanja zote za elimu, siasa, uchumi na utamaduni. Lugha ndiyo rasirimali pekee ambayo mtu anapaswa kuitumia ili kufikia maendeleo ya kweli. Ili uweze kumtawala mtu au taifa basi mnyang’anye lugha na utamaduni wake. Hivyo basi, utandawazi umekuja na upepo mkali sana mbao tusipochukua juhudi za makusudi tutakiona Kiswahili kikitupwa baharini na upepo huo. Ili kukumbatia lugha na utamaduni wetu yatupasa kujenga ukuta imara ambao hautatikisika kwa upepo wa utandawazi. Ukuta huo basi ndiyo TASAKI ya OUT. Kupitia TASAKI, sauti ya Kiswahili itasikika ndani ya nchi, Afrika Mashariki, Afrika na ulimwengu wote.
Katika misingi hii, TASAKI imeandaliwa katika muktadha unaowapa washiriki fursa ya kumulika na kutafakari mabadiliko na maendeleo ya Kiswahili katika dunia ya utandawazi ili kuleta uhuru na maendeleo ya kweli. Aidha TASAKI imekusudia kuwaandaa vijana na wananchi wote kuutambua ulimwengu wa Kiswahili na utamaduni wake. Kwa kufanya hivi TASAKI inaotesha mbegu ambazo zitazaa matunda siku moja kwa kuisimamisha nguzo ya Kiswahili ambayo ndiyo taa ya watanzania.
Hivyo basi, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinaandaa Wiki la Tamasha la Sauti ya Kiswahili litakalofanyika Novemba 2009. Hii itakuwa ni wiki ya kitaaaluma na burudani ambayo ina lengo la kutangaza, kueneza, kuendeleza na kuinua lugha ya Kiswahili na utamaduni wake katika dunia ya utandawazi.
Tamasha hili litahusisha wanazuoni, wanachama wa Kiswahili wa Afrika Mashariki na kati, Taasisi za Kiswahili, wanafunzi wa vyuo vikuu, Sekondari, wasanii na vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni, wadau na wakereketwa wote wa lugha na utamaduni wa Kiswahili ndani na nje ya nchi.
Katika wiki ya sauti ya Kiswahili kutafanyika makongamano, mashindano ya uandishi wa kazi za kubuni kwa shule za Sekondari, Vyuo Vikuu na watunzi wasio wanafunzi. Vile vile kutakuwepo na maonesho ya Sanaa na utamaduni; mavazi ya Kiswahili, vyakula vya Kiswahili, Majigambo, Ngoma, Taarab, Maigizo, Utambaji wa hadithi, muziki wa kizazi kipya na ghani za mashairi mbalimbali.
Tamasha hili litafanyika kila mwaka katika kituo chochote cha Chuo Kikuu Huria ingawa mwaka huu 2009 Tamasha hili litafanyika katika jiji la Dar es salaam.

Kauli Mbiu ya Sauti ya Kiswahili ni kueneza lugha ya Kiswahili na utamaduni wake kwa kuipa nafasi na dhima mahususi kitaifa na kimataifa.

Mada ya Sauti ya Kiswahili 2009 ni Nafasi ya Kiswahili katika Ulimwengu wa Utandawazi.
MASHINDANO!
Mashindano ya uandishi wa kazi za kubuni yatahusisha makundi matatu
· Wanafunzi wa Sekondari
· Wanafunzi wa vyuo vikuu
· Watunzi wasio wanafunzi
MADA KWA AJILI YA MASHINDANO YA UANDISHI WA KAZI ZA KUBUNI SHULE ZA SEKONDARI
Mada zifuatazo zitazingatiwa katika utunzi wa Mashairi, Riwaya, Tamthiliya, Tenzi na Ngonjera.
1.Lugha na elimu
2.Watoto wa mitaani
3.Ukimwi
4.Mauaji ya Albino
5.Lugha na mazingira MADA KWA AJILI YA MASHINDANO YA UANDISHI WA KAZI ZA KUBUNI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU
Mada zifuatazo zitazingatiwa katika utunzi wa Mashairi, Riwaya, Tamthiliya, Tenzi na Ngonjera.
1. Unyanyasaji wa kijinsia
2. Ukimwi
3. Watoto wa mitaani
4. Imani za kishirikina
5. Lugha ya Kiswahili na utamaduni wake
6. Lugha na ajira
7. lugha na demokrasia
8. Mauaji ya Albino
9. Lugha na mazingira

MADA KWA AJILI YA MASHINDANO YA UANDISHI WA KAZI ZA KUBUNI KWA WATUNZI WASIO WANAFUNZI
Mada zifuatazo zitazingatiwa katika utunzi wa Mashairi, Riwaya, Tamthiliya, Tenzi na Ngonjera.
1. Unyanyasaji wa kijinsia
2. Ukimwi
3. Watoto wa mitaani
4. Imani za kishirikina
5. Lugha ya Kiswahili na utamaduni wake
6. Lugha na ajira
7. lugha na demokrasia
8. Mauaji ya Albino
9.Lugha na mazingira
KONGAMANO!
Hapa kutakuwa na mada za kitaaluma ambazo zitajikita katika Isimu na Fasihi ya lugha Kiswahili. Dhamira mbalimbali zitajadiliwa katika kongamano. Dhamira hizo zitajumuisha mada zifuatazo
MADA ZA ISIMU
1.Kiswahili na demokrasia
2.Kiswahili na sheria
3.Kiswahili na utandawazi
4.Kiswahili na elimu
5.Kiswahili na utamaduni
6.Kiswahili na siasa
7.Ushiriki wa umma katika michakato ya kidemokrasia
8.Lugha na shirikisho la Afrika Mashariki
9.Tafsiri na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili
10.Lugha ya Kiswahili na mahitaji maalum
11.Lugha katika sayansi na teknolojia
12.Leksikografia
13.Muingiliano wa lugha ya Kiswahili na lugha za kiafrika
MADA ZA FASIHI
14.Fasihi na masuala ibuka
15.Mikondo na mielekeo mipya katika fasihi ya Kiswahili
16.Fasihi na maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni
17.Lugha ya vijana
18.Fasihi na mazingira
19.Maendeleo ya Ushairi
20.Kiswahili na jinsia
21.Kiswahili na sanaa za maonenyesho, filamu na muziki
22.Lugha na ujasiriamali
23.Lugha na ukombozi

Washiriki wa kongamano watume ikisiri za makala zao kabla ya tarehe 20/08/2009

Washiriki wa uandishi wa kazi za kubuni watume kazi zao kabla ya tarehe 20/9/2009

Karibuni sana tushirikiane katika kuienzi, kuieneza na kuitangaza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa kitaifa

Aidha, Ikisiri zote na kazi za kubuni zitumwe kwa barua pepe na anuani zifuatazo;

1. Mkuu wa Kitivo cha Sayansi na Sanaa za Jamii
Chuo kikuu Huria cha Tanzania
S.L.P 23409
Dar es Salaam
Tanzania
Barua pepe: dfass@out.ac.tz
Emmanuel.mbogo@out.ac.tz
Simu ya mkononi: +255753420118

2. Mwenyekiti wa TASAKI
Chuo kikuu Huria cha Tanzania
Kitivo cha Sayansi na Sanaa za Jamii
Idara ya Lugha na Fasihi
S.L.P 23409
Dar es Salaam
Tanzania
Barua pepe: hadija.jilala@out.ac.tz
dijaah@yahoo.com
addhass@gmail.com
Simu ya Mkononi: +255712569555


Mzuka unapopanda mjengoni

Ni kama vile wanasema ...Jamani tokaa nje mbona husikii...
Huku mlangoni jamani ngoma nzito..hakipiti kitu hapa..kudadekiiii....


Alaa...wewe ndio unajidai thupika sio ngoja nikufuate huko huko ...zake..


Wakamdaka..shuka huku ala mbona huna adamu na mkuu wa mjengoni wewe ala shwaini



Mnamzuia mshikaji ngoja mimi niwarukie juu kwa juu nione kama mtaweza


Jamaa akaona isiwe tabu akachukua mbao...haya mzuie na hii.......mbavu zenu nyieHiy0 ilikuwa katika bunge la Korea kusini ambapo ulitokea mpambano kati ya wabunge wa chama tawala cha Grand National Party na chama kikuu cha upinzani Democratic Labour Party ambao walikuwa wanazuia kupitisha kwa sheria mpya.Pamoja n jitihada zote hizo mwisho wa siku sheria hiyo iliweza kupitishwa.
VIPI HAPO WA MJENGONI....??
Picha kwa hisani kubwa ya Daily Maily uk.



Wednesday, July 22, 2009

Mweusi wa kwanza kuandika historia Miss England


Huyu ndie mweusi wa kwanza kuukwaa Miss England.Rachel Christie 20 ameukwaa ulimbwende huo jana usiku katika Hotel ya Metropole Hilton London.Tumtakie kila la kheri.

Thursday, March 12, 2009

CHAN 2009 na "Sinema" mpya

Michuano ya CHAN 2009 imemalizika huko Ivori Coast kwa Bingwa kuwa DRC Congo baada ya kumzabua Ghana 2-0 hivyo kuwa mabingwa wa michuano hiyo mipya kabisa barani Africa.
http://http://www.cafonline.com/competition/african-nations-championship_2009/results-standings
Tanzania tu mojawapo ya timu au nchi zilizoshiriki na kushia hatua ya makundi kwa kupata pointi NNE ambazo hazikutosha kutupeleka mbele zaidi.

Tulienda katika michuano hii natumaini tukiwa ni nchi pekee Afrika ambayo timu yake ilianza kujengwa muda mrefu sana toka tunaanza mbio za Ghana tukachemsha tukaja nayo pia na mbio hizi za kombe la dunia 2010 na mataifa ya afrika Angola tukachemsha(nimetaja michuano mikubwa tu ...acha chalenji).

Angalau tukagangamala kwenda CHAN.Huko nako hadithi ndio kama hiyo ikiambatana filamu za CHUJI NA BOBAN AIRPORT.Bado tunatoa vijisababu kibao.

IKUMBUKWE kuwa hatukustahili hizi pointi nne tu TULISTAHILI UBINGWA.

Nasema hivi kwa sababu timu yetu muda mrefu imekuwa kuwa inashiriki mashindano mbalimbali tofauti(toka hatua za mtoano Ghana na world cup 2010) sisi tupo tunatolewa hapo tuaingia hapa....angalia tulipo kwama http://http://www.cafonline.com/competition/african-cup-of-nations-angola_2010/news/2227-groups-and-standings-wc-south-africa-acn-angola-2010.html hivi kweli tulistahili haya matokeo pamoja na kuwachachafya Cameroon??Muda wote Kocha ameshindwa kweli kuwa timu ambayo ingekuwa tishio CHAN kweli?

Wenzetu wachezaji wao wengi hawakuwepo wako ulaya na kwingineko.angalia zambia http://http://www.fifa.com/worldcup/preliminaries/africa/teams/team=43891/statistics.htmlHapa inaonyesha kuwa bado tuna tatizo la kimsingi kabisa mipango yetu bado ni midogo au haipo.
TFF na hao wanaosimamia timu yetu hawajatupa kile tunachokihitaji kwani timu yetu ilienda ikiwa na uzoefu wakutosha kabisa Kocha wetu nae anakuwa mswahili sasa muda wake ukiihsa asipewe nyongezqa tena WAJE wengine nao watutoe hapa tulipo.

Pia uongozi wa shirikisho la soka nao waache tabia hii ya kusubiria wasamaria wema tu ndio wajitokeze wawalipie kocha muda huu ni muda mzuri wa kufunga "ndoa" na mtu utakae kuwa na sauti nae yaani utakaye weza kumwondoa muda wowote ule.Huyu lwa kuwa ni wa mjomba ndio maana mnakuwa wanyonge hamzungumzi lolote mpo tu kwa vile mnatakiwa kuwepo.Muache tabia fanyeni kazi yenu mtuletee kocha sio ilimradi kocha.

Tujiulize tumekosa kufanya vizuri kwenye mshaindano mangapi mpaka sasa?????????
Kila siku uzoefu hatuna mpaka lini wakati ni sisi kati ya timu zote ambao timu yetu imecheza muda mrefu kuliko wenzetu....HILI TUMELIFUMBIA MACHO...tuliangalie na hili...

omba nazidi kuomba

Tuko na maisha yanaendelea kwa mtindo ule ule.Usiniambie ni upi tena ?
Kwani weye hujui mtindo wetu ni kuomba.
Mara jirani mtoto katumwa mboga za kumalizia ugali....jiulize huo ugali wenyewe upo?
Ndio hivyo mwendo mdundo..ukitoka nje lifti inabidi uombe ili mambo yaende. dukani kwa mangi napo naomba nanii..Nini sema...
Kwa mwenye nyumba nako lazima landlord umwombe japo kaa muda umsawazishie mambo yake.Duu kila kona ..
Mambo yamekuwa magumu na huu uchumi...
Kwa mjomba nako kwa mbali tunasikia kilio nae anajipiga analia mambo si mambo nae anaomba aa
Sasa sijui itakuwaje jamani maana nalimtegemea mjomba nae ndio hivyo.
Daah basi tena