..................................
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Bungeni Leo katika kipindi cha maswali na Majibu kuwa Serikali imesitisha kutoa tamko lake kuhusiana na mgomo wa madaktari kama alivyoahidi jana Bungeni kuwa Leo watakuja na tamko la serikali.
Alizungumza hayo kufuatia Swali aliloulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh.Freeman Mbowe,alietaka kufahamu serikali ina mpango gani na kumaliza mgomo huo unaotesa mamia ya Wananchi.
Alizungumza hayo kufuatia Swali aliloulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh.Freeman Mbowe,alietaka kufahamu serikali ina mpango gani na kumaliza mgomo huo unaotesa mamia ya Wananchi.
Akijibu swali hilo Alisema serikali imeaanza kuchukua hatua za dharula za kuwaita madaktari waliostaafu kuja kujaza nafasi zilizowazi kwa sasa na wengine wanatoka katika Hospitali za Jeshi.
Pia wagonjwa wanaweza kwenda Hospitali ya Lugalo kupata matibabu.
Mh.Pinda pia aligusia suala la kutekwa kwa Dr.Ulimboka kuwa hata yeye taarifa hizo alizipata akiwa bungeni jana na amemtakia kupona haraka.
Serikali pia imevitaka vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi haraka ili kuweka wazi nani wanahusika na jambo hilo.
Post a Comment