Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

DK.MGIMWA:SIJUI KWANINI WATANZANIA NI MASIKINI

WAZIRI wa Fedha Dk. William Mgimwa, amesema hajui kwanini Watanzania ni masikini. Amesema kutokana na hali hiyo Wizara yake imeandaa mpango kabambe wa kukabiliana na umasikini, kupitia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini namba mbili (MKUKUTA II). 
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari, baada ya kuzindua mpango huo ambapo alisema, Serikali kupitia mpango huo itakuwa inafanya kazi ya kufuatilia kero za wananchi moja kwa moja.

Dk. Mgimwa, alisema ili kwenda sambamba na kukua kwa uchumi na kwa kuwa na mipango kabambe ya kuinua uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Pamoja na hali hii, lakini bado umasikini umepungua ambapo katika kipindi cha miaka kumi, ulikuwa asilimia 35.6 hadi kufikia 33.4, ikiwa ni tofauti ya asilimia 2.1 kupungua kwa umasikini nchini.

“Kiwango hiki ni kidogo mno na sasa tumejipanga kupitia programu hii, hakika tunafikia malengo ya kumkomboa Mtanzania wa kawaida. Na kupitia MKUKUTA II, sasa tunakwenda hadi chini na kusikiliza kero za wananchi na kuweza kuzitatua kwa wakati kama ilivyoelekezwa.

“Tunajua Watanzania wengi wanaishi Vijijini na tunatakiwa kupitia MKUKUTA II, tutarekebisha miundombinu ya vijijini sambamba na kutoa pembejeo za kilimo,” alisema Dk. Mgimwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi anayeshughulika na kuondoa umasikini Anna Mwasha, alisema uzinduzi huo utakuwa na ufuatiliaji wa kina hasa katika kulisaidia Taifa katika utekelezaji wa sera na mikakati ya Serikali kwa wananchi wake.
Chanzo:Mtanzania
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top