Na Bosire Boniface, Wajir
Benjamin Waitathu Gikonyo alinunua gari aina ya Toyota Voxy rangi ya
fedha mwezi Agosti uliopita kutoka kampuni ya Resma Motors mjini Nakuru
Mkoa wa Bonde la Ufa nchini Kenya.
Ili kujilinda uwezekano wa kuibwa na wezi, Gikonyo alinunua kifaa cha
mfumo wa usalama kinachowawezesha wamiliki wa magari kutumia simu za
mkononi kuzisimamia na kuzifanya gari zisiweze kufanya kazi iwapo
zitaibwa.
Alisema kuwa ulikuwa uamuzi mzuri wa kuwekeza katika kifaa cha
kufuatulia kwa sababu hapo tarehe 6 Novemba alipeleka ripoti katika
kituo kikuu cha polisi kuwa gari yake ilikuwa imeibwa. Kwa kutumia mfumo
wa usalama katika simu yake ya mkononi, Gikonyo aliweza kuifuatilia
gari yake hadi huko Msitu wa Ngong Patakatifu karibu na mpaka wa
Nairobi.
"Polisi na kampuni ambayo iliweka kifaa walinifuata hadi sehemu husika
na kuipata gari yangu, Gikonyo aliiambia Sabahi. "Chombo kilipelekwa
katika kituo cha Polisi cha Ngong na wahusika wanafanya uchunguzi ili
kuweza kuwakamata wahalifu."
Gikonyo alisema kuwa teknolojia hiyo ilimuokoa uchungu wa kupoteza gari
lake ambalo alinunua kwa shilingi milioni 1.2 (dola 14,000).
Wizi wa magari wapungua kwa asilimia 70 tangu mwaka 2010
Naibu msemaji wa polisi Charles Owino alisema kuwa ufuatiliaji vyombo
kwa kutumia simu ya mkononi umesaidia kupunguza takriban asilimia 70
nchini kote katika miaka miwili iliyopita na kufanya kuwa ni kizuwio na
kupelekea kutiwa mbaroni kwa watu wengi.
Kabla ya kufika kwenye soko la ndani kwa vifaa vya usalama
vinavyodhibitiwa na simu mwaka 2011, wastani wa magari 15 yalikuwa
yanaibwa kila siku nchini Kenya, aliiambia Sabahi. Sasa wastani huo
umepungua hadi magari matano.
Pia, uchunguzi zinazopelekea kutiwa
mbaroni kwa wezi zimeongezeka kutoka asilimia 10 mwaka 2010 hadi
asilimia 60 hadi sasa mwaka huu, Owino alisema.
"Mapinduzi ya simu za mkononi yamefanya kupambana na uhalifu kuwa rahisi
zaidi sasa kwa sababu ya kuwepo kwa ushahidi wa kumtia mtu hatiani,"
alisema.
Ingawaje wizi wa magari umepungua, wizi wa pikipiki umeongezeka katika
kipindi hicho hicho, Owino alisema, akiwataka watoa huduma kuingiza
sokoni vifaa kama hivyo kwa ajili ya wamiliki wa pikipiki pia.
Mwishoni mwa mwaka 2010, wizi wa magari ulihusika na upotevu wa shilingi
bilioni 2.4 (dola milioni 28), na kufanya kuwa uhalifu mkubwa zaidi
unaohusiana na mali za watu nchini Kenya, kwa mujibu wa Stephen Wambugu,
wakala wa Shirika la Bima la Milltec, watoaji huduma nchini kwa ajili
ya Kampuni ya Africa Merchant Assurance ya Kenya.
"Kwa sababu ya hali hiyo, makampuni ya bima yalillazimika kuongeza
malipo ya bima zao za gari, lakini katika miaka miwili iliyopita
imepunguka," aliiambia Sabahi.
Vifaa vya ufuatiliaji vinapunguza mzigo wa kifedha kwa makampuni ya bima
na vinawaokoa wakati wa wamiliki wa mali kutoka kazini na kuanza
kushughulika na polisi na makampuni ya bima, alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Garissa Mohammed Maalim alisema kuwa kifaa hicho pia
kinahudumu kama kizuwio kwa wahalifu. "Wanaweza kuogopa kukamatwa kwa
sababu maficho yao yanafuatiliwa, jambo ambalo pekee limeweza kuchangia
katika kupungua kwa wizi," alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa teknolojia sio hakikisho; kumekuwepo na kesi
ambapo gari zilizoibwa hazikupatikana licha ya kuwekwa kwa mifumo ya
ufuatiliaji.
Vifaa vya usalama kwenye simu vyawapa madereva udhibiti
Kampuni ya Sunrise Tracking Limited ni moja kati ya makampuni matano
yanayoweka vifaa hivi, vinavyogharimu baina ya shilingi 10,000 (dola
118) na shilingi 30,000 (dola 353) kutegemea na mtoa huduma hiyo.
Mfumo huo wa usalama ni pamoja na teknolojia ya kuonekana kitu kilipo
duniani ambacho kinawasaidia watumiaji kugundua wapi vilipo vyombo vyao.
"Teknolojia hii inawaruhusu wamiliki kupelekewa taarifa wakati matukio
yasiyotarajiwa kama vile ajali au kuingiliwa nyumbani kunapotokea,"
mkurugenzi mtendaji wa Sunrise Tracking Kelvin Macharia aliiambia
Sabahi.
"Ikiwa mwizi anavunja chombo, vifaa vya kuhisi vinatambua tukio hilo na
hutuma tahadhari katika simu ya mwenye chombo. Mmiliki anaweza kuita
vyombo vya kusimamia sheria, jambo linaloweza kupelekea kutiwa mbaroni,
au wanaweza kukifanya chombo kisifanye kazi kwa kutuma ujumbe," alisema.
Teknolojia hii pia inawaruhusu wamiliki kuangalia hali ya betri ya gari
yao na mfumo wa kiyoyozi wa gari, na hata kusikiza mazungumzo ya watu
waliomo katika gari, alisema.
Macharia alisema kuwa zaidi ya wateja 300, wakiwemo watu binafsi na
mashirika, wamenunua mfumo huo tangu kampuni yao ilipoanza kutoa huduma
hiyo mwezi Januari 2011.
Kampuni ya Mbetsa Innovations Limited pia inatoa teknolojia kama hiyo.
"Kwa vile teknolojia hii ni mpya kabisa katika soko, wateja wamekuwa
wakiongezeka kwa kasi," alisema Morris Mbetsa, ambaye anaongoza kampuni
hiyo.
Mbetsa aliiambia Sabahi kuwa kila chombo kinapewa nambari tofauti ili
kuhamasisha na kuifanya gari isiweze kufanya kazi ikiwa imeibwa. Watoaji
huduma na wanaofunga vifaa hawawezi kupata habari hii.
Ingawaje kumekuwepo na vifaa vingine vya kufuatilia katika soko, alisema
teknolojia inayohusiana na simu za mkononi ndiyo pekee ambayo
inamruhusu mmiliki wa gari kuwa dhamana mwenyewe.
Chanzo: sabahionline.com/
Post a Comment