Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela
................
Watu wawili wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kukutwa
wakiiba fedha kwa kutumia kadi 30 kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM)
ya Benki ya Afrika (Boa) eneo la Sinza jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kadi hizo ni za wateja mbalimbali wa benki ya Barclays na walitaka kuiba fedha hizo kwa kutumia kadi hizo katika benki ya Boa.
Kamanda Kenyela alisema watuhumiwa hao ambao walikamatwa jana saa 6:00 mchana, wametambuliwa kuwa ni raia wa Msumbiji lakini hakuwataja majina yao.
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanaojihusisha na wizi wa namna hiyo.
Aidha, Kamanda Kenyela alisema wizi kama huo wa kutumia mashine na kadi za benki, umekuwa ukitokea mara kwa mara jijini Dar es Salaam.
Alisema wengi wanaoibiwa fedha katika mashine za ATM, hawana uelewa wa kutosha namna ya kuzitumia hivyo kuwalazimu kuomba msaada kwa jirani, jambo linalowasababishia kuibiwa namba za siri na hatimaye kuibiwa.
Kamanda Kenyela aliongeza kuwa wizi mwingine ulitokea mwaka jana ambapo watuhumiwa wawili raia wa kigeni walikamatwa wakiwa na ATM walizokuwa wakizitumia kuibia fedha.
Mei 29 mwaka jana, Polisi jijini Dar es Salaam walimkamata raia mmoja wa Bulgaria, ambaye alinusurika kuuawa na wananchi baada ya kudaiwa kuiba dola za 23,000 za Marekani kwenye ATM.
Tukio hilo lilitokea katika benki ya Standard Chartered, tawi la Ilala jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, mtuhumiwa huyo aliokolewa na askari waliokuwa doria.
Na katika tukio lingine, mfanyabiashara Goodluck Maira (28), alitiwa mbaroni eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam akiwa na noti bandia ambazo kama halali, zingekuwa na thamani ya Sh. 720,000.
Kamanda Kenyela alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi saa 6:00 mchana.
Alizitaja namba za noti bandia alizokutwa nazo kuwa ni BU 3278825, BU 3278826 na nyingine zilikuwa zimechapishwa kwa mtiririko huo huo hadi namba 29 na kujirudia rudia.
Aliongeza kuwa mbali ya mtuhumiwa huyo mkazi wa Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam kukamatwa na noti hizo bandia, pia alikutwa akiwa na kadi mbambalimbali za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine na inawezekana alikuwa akizitumia kwa utapeli.
Kamanda Kenyela alisema mtuhumiwa huyo alikuwa na wenzake wawili katika gari aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T330 CCP.
Hata hivyo, alisema wenzake hao wawili majina yao hayakufahamika kwa kuwa walikimbia baada ya mwenzao kukamatwa akiwa anatapeli Sh. 400,000 kwenye duka la Wakala wa Huduma za M-Pesa na Tigo Pesa, Makazi Hussein (21).
“Kijana huyo alifika akiwa na wenzake wawili kwenye gari nyeupe aina ya Toyota Cresta na kuliegesha pembeni mwa duka hilo. Ndipo Maira alipoingia kwenye duka hilo alimuomba wakala amrushie Sh. 400,000 kwa M-Pesa kupitia namba ya simu 0753 898381.
Alifafanua kuwa baada ya kurushiwa kiasi hicho cha fedha, alitaka kukimbia kabla ya kumkabidhi wakala kiasi cha fedha alizorushiwa.
Hata hivyo, alisema alipotaka kuondoka huku akizozana na wakala wa M-Pesa, baadhi ya wananchi waliokuwa karibu, walimkamata lakini wenzake wawili walifanikiwa kukimbia.

CHANZO: NIPASHE
Post a Comment