Baada ya ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Gendarmerie, Wekundu wa Msimbazi wanatajiwa kutua nchini kibabe.
Simba SC ilikuwa nchini humo kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF dhidi ya Gendarmerie na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1 – 0 bao likifungwa na mshambuliaji wao raia wa Uganda, Emmanuel Okwi katika kipindi cha pili.
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo umeseme kuwa Simba itaondoka Djibouti majira ya saa 12:05 jioni.
Kikosi cha Simba kurejea leo nchini.
Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini Djibouti saa 12:05 jioni ya leo kurejea nchini kwa kutumia usafiri wa ndege kupitia Shirika la KQ.
Simba SC imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya kuifungashia Gendarmerie kwa jumla ya mabao 5 – 0,na sasa itakwaana na Klabu ya Misri.
Post a Comment