Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

PROF.LIPUMBA AKANA KUHUSIKA NA VURUGU CUF


Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ktk mkutano wa CUF na kuletea kusitishwa kwa mkutano huo.

Akijibu maswali kadhaa ya mwandishi wa Habari wa Azam Tv,Prof.Lipumba anasema ni kweli yeye kama mwenyekiti aliyejiudhuru hakualikwa wala hana vigezo vya kuingia ktk mkutano huo,lkn akiwa nyumbani alipata ujumbe wa simu ya mkononi kuwa anahitajika ukumbini na baadhi ya wanachama wanataka arudi katk nafasi yake.

Baada ya kupata ujumbe huo,Lipumba aliamua kuondoka nyumbani kwake na kwenda ukumbini,ambapo kimsingi kikatiba na kikanuni hakuwa na ruhusa ya kuingia,lkn kwa nafasi yake ktk chama alipaswa kuruhusiwa kuingia japo walinzi walimgomea wakisema haitajiki kwa muda huo,yeye alilazimika kuhakikisha anaingia ili kuweza kukidhi kiu ya wanachama waliomhitaji na wanaoona anafaa kurudia nafasi yake.

Prof Lipumba anasema hakuna mwana-CUF anayeijuwa CUF kama yeye na wala hakuna mwana-CUF toka Tz bara na hata visiwani ukitoa Maalim Seif aliyeweza kuwatetea Wazanzibar kama yeye,akitolea mfano wa kudai haki ya mwaka 2001 na harakati nyingine za kuwasemea na kuwatetea Wazanzibar.Lipumba anasema yeye ndiye kiongozi aliyezunguka Tz bara na visiwani na kufahamiana na viongozi wa ngazi zote na ndio hao wanaomtaka arudi ktk nafasi yake.

Akijibu swali la kuwa "anatumiwa na Watu kuivuruga CUF"...Prof Lipumba anasema hawezi kuihujumu CUF kwa sabbu yeye ndio sehemu ya waasisi wa chama hicho na amekipigania kwa miaka mingi ndani ya jasho na damu,hivyo kuwataka viongozi wa CUF Taifa kutumia hekima na kuacha maamuzi ya wanachama wanaotaka yeye arudi na kuchukuwa nafasi yake na kuendeleza harakati za kuindoa CCM madarakani kuelekea 2020.

Prof anasema bado ana imani kuwa wanachama wanataka yeye arudi na ndio maana hata baada ya kuwa yeye si sehemu ya mkutano kikatiba na kikanuni,bado kuna wanachama walimpigia si
mu afike ukumbini na kujuwa hatima yake ya kurudia nafasi yake.

SOURCE:JF

MAMBO 15 YALIYOTOKEA KWENYE MKUTANO MKUU WA TAIFA WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) JANA, 21 AGOSTI 2016.


  Picha mbili za kwanza zinamuonesha Ofisa wa Juu wa Polisi (mwenye shati ya kitenge) akimsaidia Lipumba na mabodigadi wake kuvamia Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF.


 Picha ya pili na ya tatu zinaonesha wajumbe Mkutano Mkuu wa CUF wakihesabiwa ili kuamua ikiwa Lipumba ANAONDOKA au ANABAKI.


Na. Mtatiro J
1. Akidi ilitimia pande zote, Bara na Zanzibar na mkutano ulimchagua Ndugu. Julius Mtatiro kwa kura takribani 500 kuwa Mwenyekiti wa Kikao, alifuatiwa na Ndugu. Ridhiwani wa Morogoro aliyekuwa na kura takribani 170 na hivyo ndugu Mtatiro alipitishwa rasmi kuongoza mkutano.

2. Mkutano Mkuu kwa kauli moja ulipitisha ajenda mbili: Moja ni Taarifa ya Barua ya Kujiuzulu kwa Prof. Lipumba na mbili ni Uchaguzi wa Kujaza nafasi wazi za Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa na Wajumbe wanne wa Baraza Kuu.

3. Mkutano Mkuu ulianza ajenda ya kwanza chini ya Uenyekiti wa ndugu Mtatiro ambapo Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alipewa ruhusa ya kueleza taarifa ya kujiuzulu kwa Prof. Lipumba na alieleza jambo hilo kwa kina, hatua kwa hatua.

4. Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF wapatao 10 kutoka Tanzania Bara walitoa hoja zao kwa kutaka Kikao kimuite Prof. Lipumba ili aje ajieleze kuhusu kujiuzulu kwake jambo ambalo lilipingwa na wajumbe wengine. Mwenyekiti wa kikao aliwataka wajumbe wanaotaka Lipumba aletwe waweze kueleza kifungu cha katiba au kanuni kinachotaka Kiongozi aliyejiuzulu yeye mwenyewe aitwe kujieleza, wajumbe hao walishindwa kutoa mamlaka ya kikatiba au kikanuni. Wajumbe waliokataa Prof. Lipumba kuja mkutanoni walinukuu ibara ya 117(2) ambayo inataka taarifa ya kujiuzulu kwake ndiyo ipelekwe kwenye mkutano mkuu na siyo yeye mwenyewe. Mwenyekiti wa kikao aliujulisha mkutano kuwa Prof. Lipumba si mjumbe wa kikao kwa hiyo hawezi kuitwa kwa sababu yoyote ile na kwamba mkutano ujadili barua zake na ufanye maamuzi ya kumrudisha au kutomrudisha.

5. Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF kutoka Tanzania Bara walikataa Mkutano Mkuu usifanye maamuzi yoyote. Wajumbe wengine wa Bara walitaka maamuzi yafanyike, kwa hiyo Tanzania Bara iligawanyika nusu kwa nusu kwenye jambo hilo. Hofu ya wajumbe wa Bara waliokataa maamuzi yasifanywe ilikuwa ni kuwa yakifanyika yataathiri mipango yao.

6. Majira ya saa 8 mchana wakati mkutano ukiendelea na baadhi ya wajumbe wa bara wakiomba mkutano mkuu umuite Prof. Lipumba, ndipo Profesa alipojitokeza akiwa na kundi la MABAUNSA wapatao 30 wakisindikizwa na Ofisa wa POLISI aliyekuwa na RADIO CALL (Angalia picha ya ukurasa wa mbele gazeti la Mtanzania). Kundi hilo liliwazidi nguvu walinzi wapatao 10 waliokuwa kwenye lango kuu na hivyo Prof. Lipumba akaingia mkutanoni kwa nguvu na kuketi upande mmoja na "genge" lake. Baadhi ya wajumbe wa bara wapatao 150 hivi kati ya 320 waliohudhuria walisimama na kushangilia ujio wa Lipumba kwa dakika kadhaa. Mwenyekiti wa Mkutano aliwatuliza 

7. Mwenyekiti wa Mkutano aliwajulisha wajumbe kwamba kwa hatua iliyopo lazima wafanye uamuzi aidha wa kumrejeshea uenyekiti Lipumba au kumuondoa kabisa, kwa kupiga kura. Wajumbe walewale takribani 150 wa Bara waliendelea kupinga kitendo chochote cha kupiga kura, wakitaka mkutano mkuu umuidhinishe Lipumba kurudi kwenye uenyekiti "kienyeji" na bila kutumia kura.

8. Mwenyekiti wa Mkutano alitoa OPTION ya pili kwamba Mkutano Mkuu uache ajenda ya kwanza uhamie ajenda ya pili na kufanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa chama na ule wa wajumbe wanne wa baraza na kwamba Mjadala juu ya Lipumba uahirishwe na pia uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti uahirishwe. Wajumbe wa bara walewale takribani 150 kati ya 320 walikataa OPTION hii ya pili wakasimama na kupiga makelele kuwa Lipumba arudishwe bila uamuzi wa kikatiba wa Ibara ya 112.

9. Mwenyekiti wa Mkutano Ndg. Julius Mtatiro aliuahirisha mkutano kwa zaidi ya saa moja ili wajumbe wakapate chakula. Katika muda huo wa mapumziko viongozi wa kitaifa wa CUF waliwasiliana na viongozi wa jeshi la Polisi kuanzia kanda, mkoa, wilaya ili kujua ni kwa nini polisi waliokuwepo walimruhusu na kumsindikiza Lipumba ukumbini na kutaka kujua ni kwa nini wanashindwa kumuondoa kwa sababu si mjumbe. Polisi walieleza kuwa wanao ulinzi wa kutosha hapo hotelini na kwamba mkutano ukirejea wataimarisha ulinzi na kuzuia makundi yoyote yasiyo wajumbe kuvamia mkutano kama lilivyofanya kundi la Lipumba na watu wake. Polisi walikataa katakata kumuondoa Lipumba na genge lake ukumbini.

10. Mkutano uliporejea, Mwenyekiti wa kikao aliwaongoza wajumbe kufanya maamuzi ikiwa LIPUMBA aondoke au abaki kwa mujibu wa katiba ya CUF ibara ya 117 (2). Wajumbe takribani 150 wa bara walisimama na kupinga. Wajumbe takribani 130 wa bara na wajumbe takribani 340 wa Zanzibar walipiga kura na kuamua kuwa Lipumba AONDOKE RASMI. Jumla ya wajumbe waliomuondoa Lipumba ni kwa kura zilizphesabiwa rasmi ni 476 huku waliosema ASIONDOKE wakiwa 14 tu. Wajumbe takribani 150 hususani kutoka Tanzania Bara walikataa kushiriki katika upigaji kura lakini wasingeliweza kuathiri akidi au maamuzi. Baada ya uamuzi huo muhimu na ukilishwaji wa ajenda ya kwanza, mwenyekiti wa kikao alikiahirisha kwa saa nzima.

11. Kikao kiliporejea saa 1 jioni hivi, Mkutano Mkuu ulihamia kwenye ajenda ya pili ya Uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Baraza. Mwenyekiti wa kikao alimkaribisha Mwenyekiti wa Uchaguzi wa ndani ya chama Wakili msomi Awadh Said akisaidiwa na Wakili msomi Job Kralio ili waongoze shughuli uchaguzi. Wakili awadh alitoa taarifa ya utangulizi akawatambulisha wajumbe wa kamati yake na wakajipanga mbele ya wajumbe.

12. Wakati Wakili Awadhi (Mwenyekiti wa Uchaguzi) akiendelea na zoezi lake, wajumbe wale 150 wa Tanzania bara walisimama wakijaribu kuzuia uchaguzi usifanyike. Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu aliwatuliza na wakamsikiliza lakini ghafla, milango mikuu ya Blue Pearl ilivamiwa na kundi la vijana zaidi ya 200 wakitokea nje, vijana hao wavamizi ambao kwa vyovyote vile lazima walikuwa wamekodiwa kwa ajili hiyo, waliwazidi nguvu walinzi wetu wa mlangoni wakaingia ukumbini.

13. Polisi kikosi kizima waliokuwepo hawakufanya chochote baada ya hali hiyo, wameshuhudia makundi ya watu wasio wajumbe wakiingia ukumbini na wamewaacha wafanye hivyo bila kuwazuia. Viongozi wa Polisi waliokuwepo "walitorokea mlango wa pili" immediatelly baada ya kundi la wahuni kuvamia.
Kundi lile lote likawa limo ukumbini ukijumlisha na lile kundi la Lipumba na mabodigadi wake wa kukodi. Kundi jipya la wavamizi mia mbili lilianza kuleta vurumai kwa kupiga baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu (wajumbe kamwe hawakupigana wao kwa wao, hata mara moja, walivamiwa kutoka nje na wahuni na baadhi ya wajumbe kunyang'anywa viti na kupigwa au kutishiwa kupigwa).

14. Kutokana na hali hiyo majira hayo kwa mamlaka ya kikatiba aliyokuwa amepewa na Mkutano Mkuu, ndugu Julius Mtatiro aliahirisha Mkutano Mkuu wa CUF hadi itakapotangazwa vinginevyo. Baada ya kuuahirisha viongozi walilindwa na kuondoka mkutanoni kwa utaratibu na wajumbe wa mkutano mkuu wakaongezewa ulinzi wa hoteli ili wawe salama.

15. Kwa maoni yangu, pamoja na kuwa Prof. Lipumba ameamua rasmi kuingia vitani na chama chake tena kwa malengo halisi ya AJENDA NA MASLAHI YAKE BINAFSI, ukweli unabakia kuwa POLISI walikuwa ni sehemu ya Mkakati wa kuuvuruga mkutano wa CUF. Kama Polisi wangelitoa ulinzi kidogo tu, mkutano ungelifanyika na uchaguzi ungelifanyika hadi mwisho. Lakini USALITI wa LIPUMBA akishirikiana na VYOMBO VYA DOLA unaweza kuwa mzizi mkuu wa hali ya jana.

‪#‎Note‬ 1: Leo nimeelezea kwa kirefu nini kilitokea mkutanoni jana. Kesho ntaeleza maoni yangu binafsi kwa ujumla.

PROF.LIPUMBA AWEKEWA NGUMU CUF

Wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akitengua uamuzi wake wa kung’atuka kwenye wadhifa huo na kuomba kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho wamepinga hatua hiyo wakisema katiba yao hairuhusu na kwamba anakwenda kukiua chama.

Kauli za viongozi hao, zimekuja muda mfupi baada ya Profesa Lipumba kutangaza nia hiyo jana kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Buguruni huku akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kuombwa.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema Lipumba hawezi kuwa na nia njema ya kukijenga chama hicho endapo atarudishwa kwenye nafasi aliyoikataa.

“Anataka kuja kukiharibu chama,” alisema Mazrui. Alifafanua kuwa tayari chama hicho kimefanya mambo mengi bila Lipumba ambaye alikuwa anaona kila kinachoendelea, hivyo alichokisema hakina mashiko kwani CUF ilisharidhia kuitisha mkutano wa uchaguzi kujaza hiyo.

Akieleza sababu alizozitoa mwenyekiti huyo, Mazrui alisema haoni chochote cha maana. “Sababu zilizomuondoa zingalipo. Kinachomrudisha ni nini?” alihoji naibu katibu mkuu huyo.

 Alisisitiza kuwa Wazanzibari wanaendelea na mchakato wa kuidai haki yao iliyoporwa Oktoba 25 na hawana nafasi ya kushughulika na masuala yasiyokuwa na tija kwao, hivyo haoni kama kuna sababu ya kumjadili Lipumba na nafasi yake badala ya kuendelea pale walipo.

 “CCM wanaona kinachoendelea, hivyo wameona wamtumie Lipumba kuja kuharibu mipango yetu. Hatuna muda wa kumjadili.Tunataka haki iliyoporwa,” alisisitiza.

Msimamo wa Mazrui haukutofautiana sana na ule wa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Twaha Taslima aliyebainisha kuwa amesikia taarifa za kurudi kwa Profesa Lipumba, lakini haoni uwezekano huo.

“Katiba hairuhusu hilo.Hakuna kifungu kinachotoa nafasi kwa kiongozi aliyejiuzulu kurudi kwenye nafasi yake pindi atakapotaka kufanya hivyo,” alisema Taslima.

Aliielezea Ibara ya 117 (2) iliyotumiwa na Profesa huyo kuandika barua ya kutengua uamuzi wake, kuwa inatoa tafsiri zaidi ya moja hivyo kuwapo haja ya viongozi kukutana na kujadili suala hilo kabla ya kutoa maamuzi.

Kwa kuwa hakuwapo kwenye mkutano huo, Taslima alisema: “Tunahitaji kukutana haraka na kujadili. Tutafanya mkutano wetu na tutavijulisha vyombo vya habari ndani ya wiki hii.”

Taslima alisema kipindi alichoongoza kilikuwa na changamoto nyingi ambazo ni tofauti na sasa, hivyo haoni haja ya mtu mwingine kuja wakati mambo yametulia. Chama hicho kilipanga kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo Agosti mwaka huu.

Baada ya kung’atuka kwa Lipumba, Taslima alichukua mikoba yake na kukivusha chama hicho kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, pamoja na ule wa Zanzibar ambao uliahirishwa na chama hicho kususia marudio yake Machi 20 mwaka huu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya alisema upo uwezekano wa Lipumba kurudi kwenye nafasi yake kwasababu mpaka sasa haijazibwa.

“Mwenyekiti huchaguliwa au kutenguliwa na halmashauri kuu. Haikupitisha kujizulu. Barua ya kujiuzulu itaenda pamoja na hii ya kutengua uamuzi wa awali,” alisema Kambaya.

Kauli ya Lipumba
Awali, Profesa Lipumba alisema mara kadhaa amekutana na viongozi wa dini na chama pamoja na wanachama wa CUF na wote walikuwa na ujumbe mmoja tu…’rudi tukijenge chama.’

Profesa Lipumba hakushiriki mchakato wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ambao kwa upande wa Zanzibar, kutokana na hitilafu zilizojitokeza ulifutwa na kurejewa Machi 20 mwaka huu huku chama hicho kikiwa kimesusia marudio hayo.

Pamoja na hayo yote, Lipumba alisema ametafakari sana juu ya hali ya kisiasa Zanzibar na kuona umuhimu wa kutoa ushirikiano ili mambo yaende kwa manufaa ya taifa.

“Ni lazima nchi iendeshwe kwa misingi ya demokrasia ambayo itapatikana kwa umoja wetu.Nimerudi kushirikiana na wenzangu kutimiza malengo hayo ili kuchangia maendeleo ya Tanzania,” alisema Profesa Lipumba.

Lipumba aliachana na uongozi wa chama hicho, Agosti 8, mwaka jana, siku chache baada ya vyama vinavyounda Ukawa kukubaliana kumsimamisha Edward Lowassa.

Alimuandikia barua Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Shariff Hamad kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama chake kuridhia makada waliohama Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Lowassa, kupewa fursa ya kugombea nafasi za uongozi.

Baada ya kukatwa kwenye mchujo wa ndani ya CCM, Lowassa akiwa na makada kadhaa wa chama hicho akiwamo aliyewahi kuwa waziri mkuu, Frederick Sumaye, alihamia Chadema ambako alipewa fursa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kilichomo ndani ya Ukawa.

Lipumba hakukubaliana na hilo, alikaa pembeni na kuachia ngazi ingawa alishiriki tukio la kumkaribisha Lowassa ndani ya Ukawa.

Jana, wakati anatangaza kufanya mabadiliko ya kile alichokiamua miezi 10 iliyopita, hakuruhusu maswali, ila alifafanua kile kitakachofuata baada ya kuwasilisha ombi hilo, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho: “Katibu Mkuu anashauriana na wanasheria kabla suala langu halijapelekwa kwenye halmashauri kuu kama katiba inavyosema,” alisema Profesa Lipumba.

SIRI YA MAALIM SEIF KUISHI HOTELINI DAR


0D6A8296 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SIRI imefichuka kuhusu hatua ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUK), Maalim Seif Sharif Hamad, kuishi hotelini jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amekuwa akiishi katika Hoteli ya Serena jijini hapa tangu aliporuhusiwa kutoka Hospitali ya Hindu Mandal Machi 8, mwaka huu alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa ofisa wa ngazi za juu wa CUF, alishangazwa na hatua ya baadhi ya watu kuhoji kiongozi huyo kuendelea kuishi hotelini hapo.

Alisema hatua ya kiongozi huyo kuishi hotelini ni matokeo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kushindwa kutekeleza ahadi ya kumpa nyumba pindi anapokuwa Dar es Salaam katika shughuli zake.


Alisema kutokana na hali hiyo imekuwa ni utaratibu kwa kiongozi huyo kufikia katika hoteli hiyo na gharama za kuishi hotelini hapo hulipwa na SMZ kwa mujibu wa sheria.


“Tangu mwaka 2010 Maalim aliahidiwa atapewa nyumba na Serikali ya SMZ lakini hilo halijafanyika, hiyo nyumba hajapewa hadi leo ndiyo maana mara zote akija Dar hufikia hotelini.


“SMZ ndiyo wenye jukumu la kulipa na si vinginevyo, kwani hata kama kama kuna viongozi wa SMZ wamepewa nyumba kwa muda wote, lakini Maalim Seif hajapewa, sasa kama unataka kujua kwa undani unaweza kuwauliza viongozi wa Serikali wao ndiyo wenye majibu zaidi,” alisema ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.


Gharama zilizotumika kwa siku 7
Kwa mujibu wa chumba anachoishi kiongozi huyo chenye hadhi ya rais ambacho hutozwa kwa Dola za Marekani 2,801.50, ambapo dola moja ni sawa na Sh 2,180. Hivyo kwa siku saba hadi kufikia leo Serikali imemlipia Maalim Seif,  Sh milioni 42.946.


Kauli ya CUF
MTANZANIA ilipomtafuta Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Hamad Masoud Hamad, alisema hatua ya Maalim Seif kuishi hotelini inatokana na maagizo ya daktari wake ambaye amemtaka apumzike kwa sasa.


Alisema kutokana na hali hiyo baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali alipokuwa akipatiwa matibabu alikwenda katika Hoteli ya Serena anapofikia kila mara anapokuwa jijini Dar es Salaam.


Alipoulizwa ni nani anayelipa gharama za kuishi hotelini hapo, Hamad alisema wanaoweza kuzungumzia suala hilo ni viongozi wa SMZ.


“Magufuli (Rais), alipokwenda kumwona alimuuliza ni nani anayemlipia gharama za hoteli na Maalim alisema wazi ni SMZ, lakini ninachotaka kuwaambia Maalim Seif hana nyumba Dar es Salaam.


“… kama wapo viongozi waliopewa nyumba wa SMZ ni hao lakini si Maalim Seif, tangu mwaka 2010 hana nyumba na hufikia hotelini, hana nyumba ya Serikali wala yake binafsi,” alisema Hamad.


SMZ wazungumza
Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema Maalim Seif anastahiki zake kama kiongozi wa SMZ ikiwemo kupatiwa haki ya matibabu pamoja na mahala pa kuishi.


“SMZ ni wajibu wake kuwahudumia viongozi na wananchi wake kwa ujumla, Maalim Seif bado ni Makamu wa Kwanza wa Rais hivyo ana wajibu wa kuhudumiwa.


“Na katika hili anahudumiwa na SMZ ikiwemo kulipiwa hoteli pindi awapo nje ya Zanzibar na si hilo tu pia tunahusika kumpa stahiki zake zote ikiwemo matibabu.


“Kwa kawaida pindi kiongozi yoyote wa kitaifa anapokuwa Dar es Salaam na kama hana nyumba SMZ hulipa malazi ya kiongozi wake na Maalim bado ni kiongozi na hata kama akiondoka kwenye uongozi bado anazo stahiki zake ikiwemo kuhudumiwa kama kiongozi mstaafu,” alisema Waziri Aboud.


Alisema pamoja na hali hiyo kwa sasa Serikali ya Muungano ndiyo inayolipa gharama za Maalim Seif kuishi hotelini kwa agizo la Rais Dk. John Magufuli.


Alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kusaidia kulipia hoteli anayoishi Maalim Seif inaonesha ni namna gani Serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar zinavyoshirikiana kwa dhati.


“Kwa ubinadamu wake Rais Magufuli tunamshukuru sana kwani inaonesha namna gani kiongozi huyo wa Jamhuri ya Muungano alivyo na mapenzi mema  na Zanzibar pamoja na viongozi wake.


“… ila pamoja na yote SMZ bado ina wajibu wa kutekeleza wajibu wake wa kuwatunza viongozi wake wote wakiwemo waliokuwa ndani ya Serikali pamoja na wale waliostaafu,” alisema Aboud.


Viongozi wamimika kumjulia hali
Tangu aliporuhusiwa kutoka hospitali kwa kiongozi huyo alikokuwa amelazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam, viongozi mbalimbali wamekuwa wakimiminika kumjulia hali.


Machi 9, mwaka huu Rais Dk.  John Magufuli, alikwenda  katika Hoteli ya Serena kumjulia hali kiongozi huyo.


Maalim Seif yupo hotelini hapo kwa mapumziko baada ya kutolewa hospitalini hapo Machi 8, mwaka huu alipokuwa amelazwa.


Katika mazungumzo yake na Rais Magufuli, Maalim Seif aliwawahakikishia Watanzania kuwa afya yake inaendelea vizuri na kwamba anaendelea na shughuli zake na siku chache zijazo ana matumaini ya kurejea katika hali yake ya kawaida.


Mbali ya kukutana na kiongozi huyo wa nchi, siku iliyofuata hasimu wake wa kisiasa ambaye ni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein naye alikwenda kumwona pamoja na wanasiasa mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.


Msimamo wa Maalim
Maalim Seif, amesema mikutano yake ya hivi karibuni na Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein haikuwa na agenda yoyote ya kujadili hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.


Kauli hiyo ya Maalim Seif aliitoa baada ya kuibuka minong’ono baada ya kutembelewa  na viongozi hao wa juu wa Serikali.


Hatua hiyo ya kukutana na viongozi hao ilizusha hisia kuwa huenda kulikuwa na jambo zito la kisiasa hasa ikizingatiwa kwamba zilikuwa zimebaki siku takriban 10 kufanyika kwa uchaguzi wa marudio visiwani humo ambao kiongozi huyo wa upinzani ametangaza kuwa chama chake hakitashiriki.


Maalim Seif alisema Dk. Shein alikwenda kumjulia hali kibinadamu kama ilivyokuwa kwa Rais Magufuli na watu wengine wenye mapenzi mema, hivyo hakuna haja kwa Wazanzibari kuwa na hofu yoyote.


“Tusingeweza kuzungumza lolote wakati afya yangu siyo nzuri sana. Unapozungumza mambo mazito kama hayo ya uchaguzi lazima uwe mzima kimwili na kiakili,” alisema Maalim Seif baada ya kujuliwa hali na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.


Maalim ambaye alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana alisusia uchaguzi huo wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.


Marudio hayo ni kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya awali kutokana na kile kilichodaiwa kukiukwa kwa taratibu.


Jecha na karatasi za kura
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, amesema ZEC imefanya marekebisho ya katarasi za kura na zinatarajiwa kufika visiwani humo Machi 17, mwaka huu.


Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyotolewa jana Jecha alisema baada ya kubainika kasoro katika jina la mgombea wa Chama cha ADA-TADEA, ZEC imefanya marekebisho.


“Tunaishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mashirikiano iliyoyaonesha katika kusahihisha kasoro zilizojitokeza na tunapenda kuwahakikishia wananchi na jumuiya za kimataifa kuwa uchaguzi utakuwa wa haki, huru na uwazi,” alisema Jecha katika taarifa yake.

CHANZO:MTANZANIA

MAALIM SEIF AWATOA HOFU WAZANZIBARI


IMG_0140 

* Azushiwa kifo, baadhi ya watu wazimia

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

ALIYEKUWA mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amewatoa hofu Wazanzibari kuwa bado yupo hai na afya yake imeimarika.

Ametoa kauli hiyo Dar es Salaam jana, baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yuko mahututi, huku mingine ikidai amefariki dunia.
Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alizidiwa ghafla juzi akiwa kwenye ndege wakati akitoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam.


Uvumi huo umekuja zikiwa zimebaki siku 10 kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, baada ya ule wa awali kufutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), mwaka jana.


Kuenea kwa uvumi huo kulisababisha vyombo vya habari kutafuta ukweli katika Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kiongozi huyo.


Ilipofika saa 7:00 mchana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CUF, Ismail Jussa akiwa na viongozi wengine mbalimbali wa chama hicho, aliwaambia waandishi wa habari kuwa Maalim Seif ni mzima wa afya.


Dakika 20 baadaye, Maalim Seif alitoka wodini alikokuwa amelazwa kwa kutumia ‘lifti’ akiwa ameambatana na daktari wake na watumishi wengine wa hospitali hiyo na kuanza kuwapungia mkono wananchi waliokuwa wakisubiri matibabu.


“Alhamdulilah, namshukuru Mungu mimi sijambo, ni mzima kabisa,” alisema huku akitembea mwenyewe bila msaada wa mtu akiwafuata wanahabari.


Akisimulia kilichotokea hadi akafikishwa hospitalini hapo na kulazwa, Maalim Seif  alisema kuwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kuja Dar es Salaam juzi, ghafla alisikia kizunguzungu.


“Namshukuru Mungu nilikwenda bara Hindi (India) kwa matibabu ambako nilifanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo na Ijumaa ya wiki iliyopita nilirudi salama na nikapokewa vizuri Zanzibar.


“Nikapumzika Jumamosi na Jumapili, siku ya Jumatatu nikaja Dar es Salaam, nimeondoka nyumbani mzima kabisa, bahati mbaya kufika ‘airport’ ghafla nikajisikia kizunguzungu, ikabidi wenzangu wanisaidie kupanda kwenye ndege,


“Tulifika Dar es Salaam salama, nikaletwa na kulazwa hapa Hindu Mandal na wenzetu walikuwa wamejiandaa vizuri, wakaanza kunifanyia vipimo,” alisema.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyomaliza muda wake tangu Oktoba, mwaka jana, alisema madaktari walichukua vipimo na kuvifanyia uchunguzi.


Alisema akiwa anaendelea kupatiwa matibabu, baada ya saa mbili kupita hali yake ilirejea kama kawaida.


“Watanzania wasiwe na wasiwasi, mimi ni mzima, nimelala vizuri, nimeamka salama asubuhi, nimefanya mazoezi na naweza kutembea mwenyewe, hali yangu ni nzuri na hata mtu akitaka tushindane kutembea hadi Kibaha naweza,” alisema na kusababisha kicheko kwa wenzake.


Alisema kuwa anawashukuru wananchi, Wazanzibari, Watanzania wa ndani na nje ya nchi ambao wameonyesha mapenzi makubwa kwake.


“Wengi walikuwa na wasiwasi na wengine waliposikia nimeumwa kiasi hicho walizirai na kupoteza fahamu, yote hiyo ni dalili wananchi wana mahaba na mimi, nami nawapenda sana,” alisema huku akisisitiza kauli aliyoambiwa na madaktari wake kwamba angeweza kupata ruhusa ya kurejea nyumbani wakati wowote jana.

DAKTARI WAKE
Daktari wa kiongozi huyo, Omary Suleiman, alisema baada ya jopo la madaktari kumfanyia uchunguzi, walibaini tatizo kubwa lililokuwa likimkabili ni uchovu kutokana na safari ndefu.


“Tulikwenda India ambako alifanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo, tukarejea salama. Juzi tulikuwa tunakuja Dar es Salaam ambako alitakiwa kuhudhuria kikao Jumatatu jioni.


“Lakini tulipofika uwanja wa ndege kule Zanzibar akajisikia kizunguzungu, hali ile ilitokea kwa sababu safari ya kutoka India hadi kufika huku ilikuwa ndefu, ilikuwa ni takriban saa sita na hakupata muda wa kutosha wa kupumzika,” alisema Dk. Suleiman.


Kwa zaidi ya wiki tatu, Maalim Seif  alikuwa nchini India alikokuwa anapatiwa matibabu na baadaye alirudi nchini na kukutana na baadhi ya wanachama wa CUF nyumbani kwake Mbweni, Zanzibar.

ATOKA HOSPITALI
Taarifa tuliozipata wakati tunakwenda mitamboni, zinasema kuwa Maalim Seif ameruhusiwa kurejea nyumbani na kutakiwa kuwa na mapumziko ya muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mawasiliano na watu wengi.


“Ameruhusiwa leo (jana) alasiri na madaktari wamemtaka awe na mapumziko ya muda mrefu, ikiwemo kutokuwa na mawasiliano na watu wengi kwa wakati mmoja na hata maongezi  kwa njia ya simu mara kwa mara,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu.

CHANZO:Mtanzania

SIKU TATU BAADA YA KUTOKA INDIA KUTIBIWA MAALIM SEIF AKUTWA NA MENGINE MAZITO


Siku tatu baada ya kutoka India alikokwenda kwa ajili ya kupata matibabu, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassoro Mazrui amesema kuwa chanzo cha Maalim Seif kulazwa katika hospitali hiyo jana asubuhi ni uchovu wa safari yake ya India ambayo alienda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.

Mazrui alikanusha taarifa zilizokuwa zinaenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kiongozi huyo wa CUF alilazwa kutokana na matatizo ya moyo. Alisema kuwa hakuna kumbukumbu yoyote ya ripoti ya daktari inayoonesha kuwa Maalim Seif ana tatizo la moyo.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CUF alisema kuwa kiongozi huyo anaendelea vizuri kiafya na kwamba hayuko katika hali mahututi kama ilivyokuwa ikielezwa.

“Anakula na kufanya kila kitu mwenyewe na hata jioni hii nimeongea naye, anakula kila kitu, hivyo Watanzania wasiwe na wasiwasi juu ya afya ya Maalim Seif,” alisema Mazrui.

Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa waliwasili katika hospitali hiyo kumjulia hali akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

MY TAKE: Kwa maoni yangu Seif Shariff anapaswa kupumzika siasa ili aangalie afya yake kwa sasa ikiwa ameukosa urais kwa awamu tano ni kheri akapumzika siasa haswa katika kipindi hiki cha ugonjwa.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui Ahojiwa na Jeshi la Polisi Zanzibar Na Kuachiwa Kwa Dhamana

Wakati polisi visiwani Zanzibar wakimhoji Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui jana, ulinzi uliimarishwa mjini Unguja huku askari wenye silaha na magari ya deraya wakifanya doria mitaani.
Mazrui, ambaye alifika makao makuu ya jeshi hilo saa 2:00 asubuhi akiambatana na wakili wake, ndiye aliyekuwa mkuu wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, ambao chama chake kinaamini kuwa kilishinda.

Barabara zinazoelekea makao makuu ya polisi kutokea Jang’ombe, Kilimani na Bomani zilifungwa huku vikosi vya ulinzi na usalama vikiwa vimetapakaa maeneo hayo na mitaa mbalimbali mjini Unguja.

Wakazi wa Zanzibar wanaojiandaa kwa uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, kuanzia Jumatano mchana walishuhudia askari wenye sare wakiwa katika magari maalumu ya kijeshi wakirandaranda kwenye barabara za Unguja, hususan mitaa ya Ng’ambo kupitia Mnazi Mmoja, Darajani, Amani, Chumbuni na Mtoni kuelekea Bububu.

Wakati hali ikionekana hivyo mitaani, Mazrui alikuwa ndani ya Ofisi ya Upelelezi ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ziwani mjini Unguja ambamo alihojiwa kwa saa tatu na nusu.

Alianza kuhojiwa tangu saa 2.00 asubuhi kama alivyotakiwa na jeshi hilo kuripoti kupitia barua ya wito aliyotumiwa hivi karibuni, hadi saa 5.30

Hata baada ya kumaliza kuhojiwa, Mazrui aliyekuwa waziri wa biashara, alilazimika kubaki kituoni hapo akisubiri kukamilika kwa taratibu za dhamana. Aliruhusiwa kuondoka saa 6.40 mchana.

Pamoja na ulinzi kuimarishwa, mamia ya wananchi, hasa wapenzi, wanachama na wafuasi wa CUF, walifika makao makuu ya chama hicho yaliyoko Mtendeni ili kumpokea Mazrui akitokea polisi.

Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mazrui alisema alihojiwa na polisi kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa Dunga Kiembeni, Wilaya ya Kati mkoani Kusini Unguja kwamba chama chake cha CUF kimechoshwa na vitendo vya hujuma na vya kihuni dhidi ya mali na ofisi zao.

“Naam, nimewaambia kwamba hiyo ni kauli yangu na niliyesema hayo ni mimi kuwa CUF tumechoshwa na uhuni huo,” alisisitiza Mazrui mara baada ya kuachiwa kwa dhamana ya masharti ya kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja wao kutakiwa kuweka hapo Sh500,000.

“Wamesema nimetoa kauli za uchochezi hivyo watanishtaki mahakamani na wamenitaka niripoti polisi Jumanne na Alhamisi.” Alisema

Mwanamkakati wa Maalim Seif Aswekwa Ndani Na Jeshi La Polisi Zanzibar

Mwanamkakati  wa aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar, Mohamed Sultan Mugheiry, maarufu kwa jina la Eddy Riyami, amewekwa ndani na Jeshi la Polisi mjini Unguja kwa tuhuma za kumtukana Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Eddy Riyami ambaye ni mmoja wa wana mkakati wa timu ya ushindi wa aliyekuwa mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alikutwa na mkasa huo jana baada ya kuitwa polisi kutoa maelezo kutokana na tuhuma zinazomkabili.

Riyami ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, alikwenda Polisi Makao Makuu kuitikia wito wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, SSP Simon Pasua, huku akiandamana na Mwanasheria wa CUF, Masoud Faki Masoud.

Mwanasheria huyo jana alisema Riyami anatuhumiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya kimtandao.

Alisema licha ya kuzikana tuhuma hizo, lakini Jeshi la Polisi bado lilimshikilia kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Ni kweli ameshikiliwa na polisi kwa ajili ya kupitisha uchunguzi na yupo Polisi Madema, eti Eddy kaambiwa kamtukana Dr. Shein kwenye ‘audio’ ambayo hata si sauti yake, lakini dhamana ipo wazi na tutamchukulia dhamana,” alisema Masoud.

Akizungumzia kukamatwa kwa Riyami, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Salum Msangi, alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Kitu ninachoweza kuthibitisha ni kuwa tunamshikilia Riyami kwa ajili ya kupitisha uchunguzi,” alisema Naibu Kamishna Msangi.

Februari 15, mwaka huu Ofisi ya Mkurunzi na Makosa ya Jinai, ilimwandikia Riyami barua ya wito na kumtaka kufika ofisi ya upelelezi iliyopo Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

Riyami alitii wito huo ambapo wiki iliyopita alikwenda lakini mmoja wa maofisa wa Jeshi la Polisi aliyemwandikia barua alikuwa nje ya Zanzibar kwa shughuli za kikazi na kumtaka kwenda jana jumatatu

Riyami si mwanachama wa CUF, lakini mara kadhaa amekuwa akitumiwa na chama hicho kwa ajili ya mikakati mbalimbali pamoja na ushauri.

MAALIM SEIF AIPONZA RADIO ZANZIBAR



NA MWINYI SADALLAH
12th November 2015
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekifungia kituo cha Radio Swahiba FM kurusha matangazo yake, baada ya kutangaza matokeo aliyotoa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Cuf, Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), akidai alikuwa mshindi katika uchaguzi uliyofanyika Oktoba 25, mwaka huu visiwani humo.


Uamuzi wa kufungiwa kituo hicho cha radio ulitolewa jana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Chande Omar, kupitia barua ya Novemba 11, mwaka huu.


“Tume kwa kuzingatia uungwana uliotumia wa kukiri kosa na baada ya kupitia maombi yako kwa mujibu wa kifungu cha 16(3) na kifungu 3(F) imetoa tahfifu ya kutopokonywa leseni na badala yake kufungiwa hadi Januari 13, mwaka,” ilisema barua hiyo kwenda kwa kituo hicho cha radio.


Chande alisema pamoja na adhabu hiyo, mmiliki wa kituo hicho anatakiwa kueleza kwa maandishi kuwa kituo chake hakitarudia tena kosa kama hilo au jingine linaloweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.


Alisema iwapo kituo hicho kitashindwa kujirekebisha pamoja na kupewa adhabu hiyo kwa kutumia kifungu cha 16 cha Sheria ya Tume ya Utangazaji ya Mwaka 2007, adhabu kali itachukuliwa.


Barua hiyo nakala yake imetumwa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, aliyetangaza kujivua wadhifa wake kwa madai ya serikali awamu ya saba imefikisha kikomo cha kuendelea kubakia madarakani Novemba 2, mwaka huu.


Nakala nyingine imetumwa kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ali Mwinyikai, pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Utangazaji Zanzibar, Abdalla Mwinyi Khamis.


Akizungumza na Nipashe jana, Mkurugezi wa Radio Swahiba FM, Khasim Suleiman, alisema wafanyakazi 24 wa kituo hicho na familia zao wameathiri kutokana na uamuzi huo wa serikali wa kukifungia kituo hicho.


Alisema walifanya juhudi mbalimbali za kufanya mazungumzo na tume lakini ghafla jana walipokea barua ya kufungiwa hadi Januari 13, mwakani.


Radio Swahiba FM ilirusha matangazo ya moja kwa moja Oktoba 26, mwaka huu, kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Maalim Seif ambaye alidai kuwa ameshinda nafasi ya urais wa Zanzibar kwa asilimia 52.87 dhidi ya mpinzani wake Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (CCM) aliyepata asilimia 47.13 katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE

SEIF PICKS NEW CABINET ,SAYS CCM HAS NOTHING TO FEAR

By Hassan Ali
Zanzibar. Opposition leader Seif Shariff Hamad yesterday said he was drafting a list of his Cabinet ministers so that they  start working as soon as he is declared the duly elected President of Zanzibar.

“I have no doubt in my mind that I’m the President-elect and only waiting to be sworn in,” said Mr Hamad, adding that he was currently putting together a line-up of ministers so that he could get down to serving the people once he is sworn in.

Mr Hamad said the government he was working on includes members from CCM as provided for in the amendment of Zanzibar Constitution that introduced the Government of National Unity in 2010.

He was addressing a meeting of Civic United Front (CUF) officials from all levels called to brief them of the developments since the surprise annulment of the election results last month.  

“I want to assure you that CUF won the elections and the ruling party defeated now all that remains is for me to be announced officially and sworn into office so that we can together build our nation,” Hamad who is the First Vice President in the outgoing government told the cheering officials.

The CUF supremo said he did not have any objection of working together with CCM as the law requires, challenging President Ali Mohammed Shein to gracefully concede defeat and name anyone else he wanted to work as his (Mr Hamad’s) deputy if he did not want to occupy that position.

“I honestly do not know what our colleagues in CCM fear because we have won 27 seats in the House of Representatives as they have. We will have the same number of cabinet ministers and lead the country together,” he said.

According to him, “the whole world knows who was elected president by the people of Zanzibar” and told the party’s officials to disregard “propaganda being peddled by CCM for a repeat election.”

Mr Hamad said there was no reason to repeat the elections as winners in all the levels were declared without any hitch. “What remains now is for the election authority to finalise the tallies for the presidency and declare the winner,” he said.

And speaking yesterday for the first time on accusations that he declared himself the winner of the October 25 election before the Zanzibar Electoral Commission Chairman Jecha Duni Jecha annulled the outcome, Mr Hamad said he would be ready to defend his stance in court.

“What I said was that ZEC ought to declare me as the winner because I won fairly. What is the problem in stating the obvious? I am ready to go to court and defend my position if anyone feels aggrieved,” he said.
While announcing the cancellation of the election results, Mr Jecha said a repeat exercise would be held in 90 days, but there has not been any signs on which way forward since then.

Several internal and diplomatic meetings have taken place to attempt to find a solution on the political crisis but no concrete steps have emerged yet. Most regional and international observers, AU, EAC, UN, US and EU countries have all advised against a repeat election and urged ZEC to conclude the tallying of the presidential vote and conclude the elections peacefully.

Unconfirmed media reports suggested yesterday that former Nigerian president Goodluck Jonathan who led the Commonwealth team of observers in the Tanzanian elections had been named mediator in the crisis.

Dr Ali Mohammed Shein whose five-year term in office expired on November 2 continues to serve in the position until the next leader is declared and sworn-in. Legal opinion remains divided whether the President was in office illegally or if the Union Constitution was also violated to allow for ascendancy of Dr John Magufuli as President despite the Zanzibar stalemate. The crisis would be Dr Magufuli’s first major test as he settles in office as Tanzania’s fifth President.


Yesterday, CUF said it would be open for any efforts to find a way out that retains the will of the Zanzibar people to determine their own political destiny.

An opposition win, they said, rekindled the hope for a better run and defended the isles of Unguja and Pemba, with the interests of the public outweighi ng  those of political leaders. “That is why we are saying there won’t any  overturning  of the wish of the people as expressed through the ballot box,” said Mr Hamad, urging that ZEC releases the tallies of the remaining 14 constituencies.

He denied ZEC claims that there had been stuffing of votes in Pemba, CUF’s stronghold. “There was not a single voting station with more than 350 voters, many had less,” he noted.

Earlier, the opposition party’s director for planning and elections Mr Omar Ali Shehe said despite the wining presidential votes, CUF also won many seat in the Parliament and in wards. He said the party raised the number of its House of Representatives in Unguja which is CCM’s stronghold from four to nine and also raised the wards from seven to 15. CUF also swept CCM out of its only three wards in Pemba and all the elective seats in the 2015 polls.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top